TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 11,005
- 22,110
- Thread starter
- #281
Asante sanaNawambiaga watu ukiwa unatafutanmaisha ukijua bado hujatusua wala huna any power nyuma yako..
Jitenge na Ndugu na wote wanaokujua yani wanaojua chimbuko lako,nenda mbali kasake maisha yako.
Kuna kitu kama hiyo inamtokea mdogo angu kwa namna yake, sababu naijua na siwezi mwambia Hachelewi niambia "kaka dunia imekuharibu" ukizingatia Asili yetu ulokole ndio kabisa.
Maisha haya ukitaka ufanikiwe kaa mbali na wanaokujua.
Watu huniambia silogeki Lakini hapana si kweli mimi ni mtu ambae sitaki kuzoeleka wala kujulikana wala ile Urafiki wa ndaniiii maana najua adui hupitia humo humo.
Watu huja serious na kuniomba niwapeleke kwa mganga wangu lakini hakuna siri kubwa ktk hii dunia kama Kuwa JESHI LA MTU MMOJA.
Wazazi,Ndugu,marafiki ni wamuhimu katika maisha yetu lakini katika upande na maswala ya mafanikio Binafsi hao watu wana asilimia chache sana za wewe kufanikiwa.
Ili ufike mbali zaidi ni lazima ujitenge na wote hao sehemu wasiokujua ANZA utaona utakavyofanya kila kitu kinafunguka.
Kuna watu wananifata PM kuniambia kila kazi wanayojaribu kufanya inakufa,biashara zina kufa Nawambiaga Hii SIRI ya kujitenga lakini wananchukulia kama nakosa cha kuwashauri, ila kuna faida kubwa sana kuishi na jamiii isiyojua wewe ni nani.
Unakua kama umezaliwa UPYA.