Tunashukuru.
Marekebisho kidogo:
neno sahihi ni shaghalabaghala, sio shagrabagra kama ulivyotumia wewe. Au nawe msamiati wa kiswahili umeenda mrama? hahhhaa.
Ila nashukuru sana kwa hilo. Sikuwa najua kuwa hiyo sentensi imerudiwa kwenye vitabu vyote vitatu. Kama kweli wewe ni mpenzi wa fasihi andishi nakushauri pia usome "The wreath for father Mayer of Masasi". Ni riwaya imeandikwa na Mtz mwenzetu S. Ndunguru. Kwa sisi tuliosoma zamani (kidato cha 4 hadi 2004 hivi) hatukuisoma. Ila sasa inasomwa shuleni. NAKUHAKIKISHIA UTAIPENDA SANA. Haina maudhui ya ukoloni, mila na desturi n.k. kama hizo za Achebe na Ngugi. Hii ina mambo ambayo ndiyo yanatokea sasa- teknolojia, dawa za kulevya na dini. Inamuhusu padre mmoja (fr Mayer), mgeni (sio Mtz) lakini anafanya kazi songea huko Masasi. Anasafiri kwenda ng'ambo kumbe anabebeshwa dawa za kulevya. Sasa endelea toka hapo...........