Chini Ya kapeti, Nyoni hakuwa na kadi 3 njano

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
Hadithi imegeuka tena .... Nyoni hakuwa na kadi tatu za njano?! ..Ngoja kwanza nimuombe Mungu azidi kunipa uhai na Movie hii katika soka la bongo nione inaishiaje!!!!!!!!??? Mtanielewa .

Walevi wanasema raha ya pombe unywe ulewe na sio kushiba au kujaza tumbo ndiii. Likithibitika hili ni kweli na Azam kurudishiwa alama zake tatu basi si vibaya hizo ofisi mkawaachia na wengine . No matter what tumejipanga na huu ubingwa.

Ilivyo sasa Azam akishinda mechi zote anakuwana 66 akiongezewa na hizi 3 atakuwa na 69. Yanga hivi sasa ana alama 68 na mechi tatu mkononi ambazo itamuhitaji alama 3 tu kuachana na mashaka haya . Hii itamfanya Yanga afikishe 72 !. Simba akimaliza zote ni 67!!.
 
Kuondoa utata na wasiwasi, Yanga angalau ipate point nne katika mechi zilizobaki.
Mpira wa Bongo huwezi kujua maana mtu alipewa ruhusa akacheze ndondo kule Zambia
 
Mechi zenyewe jumla ni chache si kazi kujua hzo kadi hebu mwenye kujua aziseme maana tunawasubiri hao TFF kama vile mechi zinachezwa gizan
 
Taarifa zilizopo ni kwamba Azam wamepeleka barua tff ya kupitia tena michezo ya azam ili kujiridhisha kama kweli alikuwa na kadi 3 za njano. Pia wamepeleka cd zote za michezo ya azam,
Hapa yanga anapaswa kushinda Game ya Jumanne dhidi ya Mbeya city ili kujihakikishia ubingwa, Maanake hawa tff hawaeleweki.
 
Zinazojiri Asubuhi hii Jijini Dar es salaam ni kuwa Mashabiki wa Simba wamejazana kwenye makao makuu ya timu yao na kinachoaminika ni kuwa mashabiki hao wanataka viongozi wa timu hiyo waachie ngazi
 
H
Taarifa zilizopo ni kwamba Azam wamepeleka barua tff ya kupitia tena michezo ya azam ili kujiridhisha kama kweli alikuwa na kadi 3 za njano. Pia wamepeleka cd zote za michezo ya azam,
Hapa yanga anapaswa kushinda Game ya Jumanne dhidi ya Mbeya city ili kujihakikishia ubingwa, Maanake hawa tff hawaeleweki.
Hapa ndipo inapokuja hoja yangu ya ukakasi wa Azam TV kupewa haki za kurusha matangazo ya Ligi ambayo timu ya kampuni yao mwenza inacheza. Ndio mgongano wa kimaslahi ambao nimekuwa nikiitetea Yanga kwenye msimamo wao wa kukataa hilo (ingawa wao wameliangalia kipesa zaidi). Angalia sasa: (1) Azam TV watakuwa waungwana kiasi gani kuonesha matokeo yatayoiumiza Azam FC kwenye video hizo? (2) Hata uungwana huo ukiwapo, Mbeya City watakuwa na imani gani kwamba Azam TV haikuchezea mikanda hiyo ili kufuta matukio ya Nyoni kuoneshwa kadi nyekundu? (3) Kwa mfano Azam TV watashinda rufaa yao kwa mgongo wa video za Azam TV, mamlaka za rufaa zitachukua sekunde ngapi kuipa ushindi Mbeya City itapotumia ukweli huo wa mgongano wa kimaslahi wa Azam TV na Azam FC?
Tujifunze. Ukupigao ndio ukufunzao!
 
Hivi kunawenye akili timamu anashabikia mpira wa Tz ?!!?? Mpk leo

Kama yupo huyo ni jasili
Huo ndio unaitwaga umbeya, ushakumbembe na ushoga kwa kifupi unatabia za kike kike...sasa kama haufatiliagi mpira wa bongo kihere here cha kusoma kufungua na kukoment kimetoka wapi???kulikuwa na ulazima wa kukomenti? C ungepotezea kimya kimya wale ambao hawafatilii mpira wa bongo hawana kihere here cha hivyo wako bize na majukwaa mengine na akiingia jukwaa la michezo ni kwenye thread za ligi za ulaya full stop
 
H

Hapa ndipo inapokuja hoja yangu ya ukakasi wa Azam TV kupewa haki za kurusha matangazo ya Ligi ambayo timu ya kampuni yao mwenza inacheza. Ndio mgongano wa kimaslahi ambao nimekuwa nikiitetea Yanga kwenye msimamo wao wa kukataa hilo (ingawa wao wameliangalia kipesa zaidi). Angalia sasa: (1) Azam TV watakuwa waungwana kiasi gani kuonesha matokeo yatayoiumiza Azam FC kwenye video hizo? (2) Hata uungwana huo ukiwapo, Mbeya City watakuwa na imani gani kwamba Azam TV haikuchezea mikanda hiyo ili kufuta matukio ya Nyoni kuoneshwa kadi nyekundu? (3) Kwa mfano Azam TV watashinda rufaa yao kwa mgongo wa video za Azam TV, mamlaka za rufaa zitachukua sekunde ngapi kuipa ushindi Mbeya City itapotumia ukweli huo wa mgongano wa kimaslahi wa Azam TV na Azam FC?
Tujifunze. Ukupigao ndio ukufunzao!

Hadi wanafikia kuipokonya Azam ushindi lazima watakuwa waliridhika na ushahidi uliokuwepo.

Kikubwa ni ripoti za waamuzi na kamisaa wa mchezo. Katika michezo yote mitatu iliyotangulia wa MCC, kama marefa walionyesha kuna kadi za njano kwa Nyoni, mikanda haiwezi kupindua hilo.

Na tukumbuke mechi za mikoani, Azam Tv hawatumii camera zote kuweza kuchukua kila tukio.
 
Sadakta. Lakini hiyo hiondoi hatia ya kuipa Azam TV haki za kurusha Ligi inayochezwa na Azam FC. Uwezekano huu wa kutumia kanda za Azam TV kusaidia kuhukumu kesi dhidi ya Azam FC ni kama kirusi kilichobainika (na baadhi yetu) kwa kutumia darubini ya tukio la Azam kunyan'ganywa pointi.
 
Hivi kunawenye akili timamu anashabikia mpira wa Tz ?!!?? Mpk leo

Kama yupo huyo ni jasili
Hivi kunawenye akili timamu anashabikia mpira wa Tz ?!!?? Mpk leo

Kama yupo huyo ni jasili
Tupo tena wengi tu na kuna wengine kina Katavi,balantanda,Sibonike bila kumsahau first lady wa yanga hapa JF Nifah yaani hutuambii kitu kwa timu zetu za nyumbani watakuja kutoa ushuhuda wao.
 
Sadakta. Lakini hiyo hiondoi hatia ya kuipa Azam TV haki za kurusha Ligi inayochezwa na Azam FC. Uwezekano huu wa kutumia kanda za Azam TV kusaidia kuhukumu kesi dhidi ya Azam FC ni kama kirusi kilichobainika (na baadhi yetu) kwa kutumia darubini ya tukio la Azam kunyan'ganywa pointi.
Mkuu, kwenye hilo tuko pamoja. Kuna conflict of interest kubwa sana.

Labda kwa sababu ya umaskini wa TFF. Hata hili la Azam huyo huyo kuwa mdhamini wa FA cup limekaa vibaya. Kuna siku TFF watalia sana.

Mfano mwingine ni ujanja wa TBL kuwadhamini Yanga na Simba. Wachukue mmoja ili Serengeti Breweries achukue mwingine ili tuone ushindani wa kweli.
 
Tupo tena wengi tu na kuna wengine kina Katavi,balantanda,Sibonike bila kumsahau first lady wa yanga hapa JF Nifah yaani hutuambii kitu kwa timu zetu za nyumbani watakuja kutoa ushuhuda wao.

Hilo halina ubishi mkuu. Huyo anatafuta sababu baada ya wamatopeni kuangukia pua kwa miaka kadhaa sasa. Shabiki wa mpira huwezi kuacha timu yako hata ikishuka daraja.
 
Back
Top Bottom