Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 992
- 2,285
Sio kwamba CCM ni chama kibaya, wala kwamba sera zake ni mbaya au kwamba watu wake ni wabaya au kwamba wanachama na viongozi wake hawana uwezo; hayo yote ni HAPANA.
Ndani ya CCM kuna watu makini, wazalendo na wenye tamaa ya maendeleo lakini wote hao wamemezwa na mfumo kwasababu nao ni binadamu
CCM ya sasa imeunganishwa na dola/serikali ambayo kimtazamo watu walioko "dolani/serikalini" hawana muda na maendeleo ya nchi wala ya watu bali maendeleo yao binafsi. Kila mmoja anashindana na mwenzake kujiimarisha kiuchumi yeye na familia yake hakuna anayejali kuhusu nchi wala watu wa nchi
CCM kama chama tawala kilitakiwa kiwe na watu wenye jicho la kuyaona haya na kuyakemea lakini isivyobahati wanayaona na kuyasifia na wale wachache wanayafumbia macho. Hii ni mbaya sana na wanafanya hivyo kwasababu nao wanatamani na wanatarajia siku moja wawe sehemu ya serikali
Hakuna kiongozi wa chama mwenye uwezo wa kumkosoa kiongozi wa serikali, hakuna mwanachama mwenye uwezo wa kumuhoji kiongozi wa serikali. Hii imepelekea viongozi wa serikali kuwa huru kufanya wanavyotaka wao
Tegemeo pekee la kuikomboa nchi hii limebaki kwa wananchi wenyewe ambao nao ni kama wameshakata tamaa
Wamekubali yaishe! Watoto wanasoma shule zisizo na miundombinu mizuri lakini wameridhika, watoto wanafaulu kwa kishindo pasipokuwa na maarifa kichwani wao wanashangilia (siku hizi ni kawaida sana kuwasikia wazazi wanashangaa alama walizopata watoto wao kwenye mitihani ya mwisho)
Wagonjwa wanatibiwa kwa manyanyaso na kulazimishwa kutoa hongo lakini hakuna anayejali, ofisi za serikali kama ardhi, TRA, manispaa nk wafanyakazi wanaviburi kuanzia kwa mlinzi/sekretary hadi kwa boss lakini hakuna anayejali
Haya yote yanahitaji check and balance ili yaende na chama kama mwajiri mkuu wa walioko serikalini kilitakiwa kifanye kazi hiyo lakini kimeshindwa.
Nini kifanyike?
Kukitoa madarakani imeshindikana na haionekani ikiwezekana, kuwabadilisha watu "mind set" ili waanze kufikiri na kutenda kwa namna ya kuwawajibisha wasiofaa bila kujali itikadi zao nayo inaelekea kufeli kwasababu siku hizi hata mtumishi wa umma akiwa na mawazo kinzani dhidi ya kiongozi wake wa kazi au kuhoji mambo ya msingi anaonekana mpinzani na inawezekana kabisa asiungwe mkono na wafanyakazi wenzake. Hii hutoa nafasi kwa Boss kumshughulikia atakavyo ili kudhibiti wengine.
Je, tuendelee kusubiri kudra za Mwenyezi Mungu?