J4 King hivi sio kwamba kuna maeneo twaweza kuruhusu wawekezaji na mengine hapana??
yaani kwetu mabo yanfanywa holeholela....hata tax driver awe mchina??? haya sisi tufanye nini sasa?? tunabaki kumangamanga ndani ya nchi yetu!!!
huyo anayesema huduma yao nafuu hebu atuthibitishie basi...
asa uhv said it ....hapa si kw amaslahi ya taifa mkubwa....pity!
Resentments za namna hiyo zitatokea tu Bongo.
Mwezi uliopita moshi ulifuka Angola:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ca-visible-at-kariakoo-market.html#post659942
This is a wake up call for everybody! Tuache kulalamika na kutumia fursa zilizopo, although i have to say kufanya competition na wachina especially kwenye biashara, tena ya vitu vinavyotoka kwao is rather difficult. Kuna nguo za watoto jamaa wanauza 2000-2500 , nguo ambayo ungeinunua kwenye duka la mbongo kwa 8000 minimum. so akili kichwani, tumieni hizo fursa kama hizo kwa kufanya biashara hata mikoani ambako hawajafika, that is just one example coz i think they are here to stay, seeing the kind of leadership we have.
I recently had a conversation na shop owner hapo Kariakoo, Mtaa wa Swahili. Jamaa wanadai wachina wanaua biashara ya knobs za draws na vitasa. Mimi mwenyewe nimeshuhudia duka moja hapo Kariakoo adjacent to Swahili street, but near where they sell electrical goods. Jamaa bei zao ziko chini kishenzi, yani huwezi kushindana nao. I didn't buy from them kwasababu najua wabongo wanahitaji biashara yangu. But with those kind of prices, I don't know how long I can hold my breath ...😕
Resentments za namna hiyo zitatokea tu Bongo.
Mwezi uliopita moshi ulifuka Angola:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ca-visible-at-kariakoo-market.html#post659942
Nakubaliana nawe. Swala la msingi sana umeeleza.Inabidi watanzania waamke, anayetaka kujua dunia inakwenda wapi ajaribu kusoma historia ya dunia kutoka katikati ya 1800 hadi hivi leo. Upepo wa mabadiliko yanayotokea leo dunia ni ya kawaida na yametarajiwa toka wakati huo. Dunia imeshafikia kuwa katika ngazi moja kama vile kijiji kwa hiyo kama tuna-resist mabadiliko tutalia kilio mbwa na kusaga meno. Tunachotakiwa si kulalamika, la hasha tuangalie na sisi tutabadilikaje kuendana na hali halisi ya mabadiliko.
Endapo mimi ninafanya kazi mwezi mzima, nitahitaji at the end of the day nifanye saving, ikiwa dukani kwa mchina anauza nguo kwa 2500/= na kwa mbongo 8000/=, sihitaji rocket science kuona ni wapi nitapa nafuu, na hii ndiyo faida ya utandawazi, wabongo wawe wabunifu kwani biashara zao zitazidi kudoda. Endapo Taxi ya mchina inatoa huduma nzuri na kwa bei nafuu, nina sababu gani ya kwenda kukamuliwa pesa nyingi kwa mbongo mwenzangu? Dunia inasonga mbele kwenye soko huria na haitarudi nyuma. China yenyewe kama nchi imeona kuwa isipofanya mabadiliko itaachwa nyuma, leo hii China ni tishio katika anga za kiuchumi wa dunia.
Kabla hatujaanza yale yalitokea hivi majuzi South Africa tujichunguze wenyewe, Leo tunawasema wachina Kesho wanaingia rasmi Wakenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Ikiwa tutaendelea kuvuta miguu tunapopewa kazi...inachukua nusu saa kuletewa kinywaji mezani unapoagiza, maofisi mahospitali kazi haziendi kwa gharama mteja anayolipia, muda si mrefu tutawakuta wafagia barabara si watanzania.
Well put!...
We don't need unskilled labor as we already have enough of those. Perhaps we should think about moving some of our unskilled labor to China; that would be cool - itapunguza msongamano kwenye magereza yetu.
Tunahitaji kuchuja Chinese criminals wanaokimbia mkono wa sheria huko watokako.
......
Nakubaliana nawe. Swala la msingi sana umeeleza.
Ila sasa, unataka tufungue milango raia wa kigeni waingie nchini wafanye kazi watakayo? Nipe majina ya nchi zinazofanya huo upuuzi.
Wenzetu wana-incourage foreign workers waende kufidia pengo la uhaba wa skilled labor kwenye maeneo maalum, mfano madaktari. Tunahitaji manesi na madaktari zaidi ili tuishi kwa afya. Tunahitaji waalimu ...kuna maeneo mengi tu.
We don't need unskilled labor as we already have enough of those. Perhaps we should think about moving some of our unskilled labor to China; that would be cool - itapunguza msongamano kwenye magereza yetu.
Tunahitaji kuchuja Chinese criminals wanaokimbia mkono wa sheria huko watokako.
Foreigners waje, wafanye kazi kwenye makampuni ya watanzania, sio waanzishe makampuni yao. Au kama ni makampuni yao (mfano kwenye construction) sheria iwalazimishe wafanye kazi jointly na locals.
Usimamizi wa sheria zilizopo ni hovyo. Wafanyakazi serikalini na taasisi zake wamekuwa mstari wa mbele kuingia ushirika na wageni kufanya mambo kinyume na sheria. Magogo kiasi gani yametoroshwa? Nyara kiasi gani wamekomba? ...You name it!
Mfano mdogo tu kuhusu sheria:
In Malaysia: Foreign workers can only work for five years
SOURCE: http://whiteglove.com.my/index.php?option=com_content&task=view&id=197&Itemid=47
Picture that! Jiulize kwa nini wenzetu wameweka sheria ya namna hiyo.
Je tatizo la msingi hapa ni nini? Je ni huyu taxi driver mchina au ofisa wa serikali aliyemruhusu kufanya hiyo biashara? Je tukiwafukuza wachina na wageni wengine wote tatizo litakuwa limekwisha? Kumbuka kwamba Dar-es-salaam ina watu wengine wengi toka nje ya nchi wakiwemo wakenya, waganda, waingereza, wacongo, wanigeria nk.
Mimi nadhani tatizo la Tanzania ni watanzania wenyewe hii inajumuisha watawala wetu na sisi watawaliwa. Soko HURIA lina taratibu zake na Serikali inatakiwa kusimamia soko hili kwa mujibu Katiba, sheria, sera na taratibu zinazoeleweka ili liweze kuleta manufaa kwa wananchi.
Kwa bahati mbaya badala ya kuanzisha soko HURIA viongozi wetu, kwa sababu zao binafsi za kifisadi, walianzisha soko HOLELA lisilokuwa na sheria wala taratibu zinazoeleweka na wala msimamizi.
Huwezi kuwa na Katiba ya nchi inayohuribi msingi wa UJAMAA halafu ukaendesha mambo kwa utaratibu wa SOKO HURIA. Huu ni mkanganyoko wa kisera na unatoa ombwe la watu kufanya mambo wanayotaka kwa faida zao wenyewe. Hivi sasa kwenye Ujamaa hatupo, kwenye Ubepari hatupo, kwenye Soko Huria hatupo - yaani tupotupo tu.
Ni lini mara ya mwisho tulimsikia kiongozi akiongelea masuala ya UKOLONI MAMBOLEO hapa Tanzania? Je ina maana ukoloni mamboleo umekwisha dunia hii? Je huu unaoitwa utandawazi siku hizi siyo ule ukoloni mamboleo ila ikiwa na sura na mavazi mengine? Tumejiandaa vipi kusimamia raslimali zetu kama nchi katika huu mfumo unaotawaliwa na ukoloni mamboleo?
Ninavyoelewa ukoloni mamboleo ni mbaya kuliko ukoloni mkongwe kwani umewageuza watawala wetu kuwa MAKUWADI wa raslimali za nchi katika soko huria.
Mimi binafsi sipingi ujio wa wafanyakazi wataalamu toka nje ya nchi ili mradi tu wazingatie sheria, taratibu na sera za nchi ambazo ama hazipo kwa sasa au zipo lakini zinaweza kubadilishwa kwa kitu kidogo. Hawa wageni ni muhimu hasa kama sehemu wanazokuja kufanya kazi zina upungufu mkubwa wa utaalam na uzoefu na kuna utaratibu wa kuwafundisha wataalamu wa nyumbani ili baadaye tusihitajike kuleta watu toka nje.