comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Salaam wana JF
Serikali ya China imezidi kuliimarisha jeshi lake la majini baada ya kuzindua meli mpya aina ya 001A lakini bado haijapewa jina maalumu,melivita hiyo itakayokuwa na uwezo wa kubeba ndege vita aina za Shenyang J-15, makombora,na vifaa vingine vya kijeshi iliobuniwa 2013 na kuanza kutengenezwa mwaka 2015 itaendelea kufanyiwa majaribio mpaka mwaka 2020 ina uwezo wa kubeba vifaa vya uzito wa tani 70000, melivita hiyo imetengenezwa nchini China kwa tekinolojia ya China inafuatia melivita nyingine ya China aina ya Liaoning ilionunuliwa miaka ya 90 kutoka Ukraine.
Hali hiyo imefuatia tishio la kiusalama kutoka Marekani katika pwani ya bahari ya kusini mwa China kitendo cha Marekani kuitishia Korea Kaskazini kijeshi, vilevile kufuatia Marekani kuweka mifumo ya kiulinzi ya makombora katika pwani ya Korea kusini inayojulikana kama THAAD, Serikali ya China na Korea kaskazini inasema inaweza kuingilia mifumo mingine ya makombora katika eneo hilo.
Uwezo huo wa kijeshi utaiwezesha serikali ya China kulinda maslahi yake ya kiuchumi hasa katika bahari ya kusini
BBC NEWS