China yaipiga nyundo Marekani

Nikilewa mniache

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
19,277
Reaction score
51,861
Baada ya siku mbili za mazungumzo jijini Stockholm, pande zote zilionyesha nia ya kusuluhisha tofauti zao lakini msimamo wa Washington wa kuitaka China kusitisha biashara hiyo ya nishati bado ni kikwazo kikuu.

Msimamo wa China wa kukataa shinikizo hilo unaangazia jinsi Beijing inavyolipa kipaumbele suala la nishati kama sehemu ya sera yake ya kigeni na usalama wa taifa.

Katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa X, Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilisisitiza kuwa "China daima itahakikisha usalama wa nishati yake kwa njia zinazolinda maslahi ya taifa,” na kuongeza kuwa "vitisho na mashinikizo haviwezi kuleta mafanikio.”

Kauli hiyo imeonesha wazi kuwa Beijing haitakubali kushinikizwa katika masuala ya nishati, na inalitazama suala hilo kama msingi wa uhuru wake wa kidiplomasia na wa kiuchumi.

Mtazamo huu wa China umekaririwa pia na Msemaji wa wizara ya mambo ya Nje ya China Guo Jiankun ambaye amesema;

"Msimamo wa China dhidi ya ushuru wa kiholela wa forodha umekuwa wa wazi na thabiti. Hakuna mshindi katika vita ya ushuru au vita ya kibiashara. Kulinda masoko kwa misingi ya kitaifa kunadhuru pande zote zinazohusika."

Washington yatishia kutumia Β΄runguΒ΄la vikwazo dhidi ya Beijing

Marekani imetishia kuiwekea China ushuru wa asilimia 100 kwa bidhaa zake kama njia ya kuilazimisha ikubali masharti ya kimataifa kuhusu ununuzi wa mafuta.

Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent, amekiri kuwa Wachina ni "wajanja” katika majadiliano, lakini ameongeza kuwa suala la mafuta halijavuruga mchakato mzima wa mazungumzo.

Hata hivyo, wachambuzi wanatahadharisha kuwa utekelezaji wa vitisho hivyo unaweza kufuta mafanikio yote ya kidiplomasia na kuharibu uwezekano wa makubaliano kati ya Rais Trump na Rais Xi Jinping.

China kwa sasa ndiyo mnunuzi mkuu wa mafuta kutoka Iran β€” ikiwa inachukua kati ya asilimia 80 hadi 90 ya mauzo ya mafuta ya nchi hiyo, zaidi ya mapipa milioni moja kwa siku.

Kwa upande wa Urusi, China ilinunua zaidi ya mapipa milioni 1.3 kwa siku mwezi Aprili pekee, kwa mujibu wa taasisi ya utafiti ya KSE nchini Ukraine.

Biashara hii ya mafuta si tu kwamba inaimarisha uchumi wa China, bali pia inazipatia Iran na Urusi mapato muhimu katika kipindi ambacho zimewekewa vikwazo na Marekani.

Wataalamu wanasema China inaamini kuwa mafuta kutoka Iran na Urusi ni nguzo muhimu kwa usalama wake wa kiuchumi na kisiasa.

Wanasiasa wa Marekani waanzisha jitihada za kuongeza shinikizo


Kutoitii Marekani kunatazamwa kama njia ya kuonyesha mshikamano na Moscow huku ikiendelea kupunguza utegemezi wake kwa vyanzo vya nishati kutoka nchi rafiki za Marekani.

Aidha, Beijing inaona sera za Marekani kuhusu Urusi na Iran kuwa zenye mgongano na zisizo na msimamo wa pamoja, hali inayoiwezesha kujadiliana kwa ujasiri zaidi.

Kwa upande mwingine, Marekani inazidi kuimarisha shinikizo kwa njia ya vikwazo. Seneta Lindsey Graham ameanzisha mswada wa sheria unaoruhusu ushuru wa hadi asilimia 500 kwa nchi "zinazojua” zinanunua mafuta kutoka Urusi, hatua inayolenga kukomesha ufadhili wa vita ya Putin dhidi ya Ukraine.

Mswada huo umeungwa mkono na wabunge kutoka vyama vyote viwili vikuu vya kisiasa nchini Marekani.

India, kama China, ni mnunuzi mkubwa wa mafuta ya Urusi. Rais Trump ametangaza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa kutoka India, akilalamikia kwamba hatua hiyo ya manunuzi ya mafuta inaifanya India kuwa miongoni mwa wafadhili wa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.



Ikulu ya Marekani imesisitiza kuwa si haki kwa mataifa kama India au China kunufaika kiuchumi huku yakiepuka matokeo ya kisiasa ya migogoro ya kimataifa.

Ingawa pande zote mbili β€” Marekani na China β€” zimeonyesha nia ya kufikia makubaliano ya biashara, mvutano kuhusu mafuta umebainisha kuwa si kila jambo linaweza kujadiliwa mezani. Kwa China, nishati si suala la kiuchumi tu β€” ni suala la msingi la usalama wa taifa.
 
USA Hachelewi Kuja Na
TARIFFS PRO MAX
Utawasikia Tu China Wakiomba Poo,
USA Wanajivunia Wananchi Wa Usa Kuwa Na Uwezo Mkubwa Wa Kuspend Hela Kuliko Nchi Yoyote Duniani (yaani Ni Watu Wa Anasa),sasa Ukipigwa Tariff Kupeleka Bidhaa USA Inakula Kwako,tofauti Na Wao Ukiwapiga Tariffs Haziwabani,maana Wana Alternatives Nyingi.
 
Kwani mataifa mengine ni mbumbumbu hawawezi kubuni an alternative means za ku-
survive au ku-kwepa vikwazo!

Halafu kitu kingine ambacho huwa kinanishangaza: Taifa la Merikani alijawahi kupewa mandate na UN kwamba
wanaweza ku-slap punitive sanctions kwa Taifa lolote wanapojisikia-yaani wana violet misingi ya biashara iliyo anzishwa na Umoja wa Mataifa baada ya WW2.

Merikani, EU na Uingereza wamekuwa majeuri sana wa kuwa vinara wa kutojari misingi ya agencies za Umoja wa Mataifa mjawapo ikiwa inahusu masuala ya ufanyaji biashara baina ya Mataifa na Mataifa - Merikani, EU na Uingereza wamekuwa kero sana kwa kutaka kupoka nguvu za Umoja wa Mataifa kuhusu masuala mengi tu moja wapo likiwa hili la SANCTIONS wanali abuse for political REASONS basi, hawana habari kwamba linaweza hata kusababisha VITA!! Mataifa ya magharibi matatizo sana.
 
Kwani alianza Jana au juzi kufanya hizo sanctions!? Mbona India na china Bado Wana endelea kununua hayo mafuta in short USA now days ni Simba wa kuchora hakuna anaye muogopa
 
Kwani alianza Jana au juzi kufanya hizo sanctions!? Mbona India na china Bado Wana endelea kununua hayo mafuta in short USA now days ni Simba wa kuchora hakuna anaye muogopa
USA Hawajaamua Kutumia Full Force Wakiamua Hivyo Hakuna Wakupinga, Huwa Wanatarget Makampuni Yanayoagiza Mafuta Hadi Mwenye Meli,hawajafikia Huko Safari Hii,
BRICS Na Umoja Wao Wako Wapi?
LAZIMA MKUBALI USA NI KAMA UPEPO YUPO HADI CHUMBANI KWAKO,NA HATA SEHEMU ZAKO ZA **
ANA MKONO MREFU SANA,NI MUNGU TU NDIO ANAWAZIDI KWA MBALI.
 
Hana huo uwezo acha uongo Yaani USA Apate chance ya kumtokomeza Russia halafu Asifanye hivyo thubutuuu Mzee acha story za vijiweni
 
Huawei sihao hapo Bado wanaendelea kuproduce bidhaa zao au una sikiliza propaganda za west?? na Wana mpaka magari yanayo tumia Umeme
Huawei Wamebaki Kwenye Soko La China Tu,wamepotezwa Nje Ya China
Ukisema Wanatengeneza Magari Ya Umeme Ujue Wameamua Kubadilisha Biashara Baada Ya Kupotezwa Kwenye Simu Nk
Halafu Suala Magari Ya Umeme Kwa China,wanaotamba Ni BYD
Na Magari Ya Umeme Kwasasa Ni Dunia Nzima Yanatengenezwa,we Hadi Kina Masoud Kipanya Nao Wanatengeneza.
 
Nikuulize swali jepesi nafikiri litafunga mjadala mzima.

Unaifahamu Huawei kama kampuni ya nini ?
 
Kwan tarrif apige mara ngapi ? Izo zilieza kufanya kazi Zimbabwe tuh
 
Mkuu haupo sahihi hata kidogo .
Huawei bado ipo xnaa alaf haitoi huduma za simu tuh
Afu Kwa taarifa yako Huawei ndio kampuni ya kwanza kuzindua 5g na mataifa mengi wanatumia huduma zao
 
HUAWEI NA ZTE Wako Wapi?
Unajua Ni Makampuni Mangapi Ya Kichina Yanakufa Kwa Vikwazo Na Bans Za USA?
Hivi unajua kuwa nguvu ya Huawei ikahamishiwa Oppo na Xiaomi?
Hapo USA amezuia nini?
Sanasana alipoipiga ban Huawei China waka retaliate kwa kuzuia Mali ghafi za viwanda na 2018 viwanda vingi vilidorora ndani ya USA
Hakuna trade war ambayo USA amewahi kushinda dhidi ya China.
Usitake kutudanganya.
 
Mkuu haupo sahihi hata kidogo .
Huawei bado ipo xnaa alaf haitoi huduma za simu tuh
Afu Kwa taarifa yako Huawei ndio kampuni ya kwanza kuzindua 5g na mataifa mengi wanatumia huduma zao
Hajui kama Huawei ni miongoni mwa makampuni Bora ya simu hadi sasa.
Na Bado wanatoa huduma kama kawaida. Ilishuka tu kwa rank ila still iko pale pale.
 
Hana huo uwezo acha uongo Yaani USA Apate chance ya kumtokomeza Russia halafu Asifanye hivyo thubutuuu Mzee acha story za vijiweni
Huyu jamaa anashangaza.
Amenishangaza aliposema Huawei imepoteza soko la dunia imebaki China tu.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Sijui anaishi dunia gani huyu jamaa!?
 
Nikuulize swali jepesi nafikiri litafunga mjadala mzima.

Unaifahamu Huawei kama kampuni ya nini ?
Swali Lako Linaonyesha Huna Imani Na Uelewa Wangu Kuhusu Haya Mambo Ya Tech Na Diplomasia Ya Kiuchumi Duniani,kwaio Hata Nikikujibu Huwezi Kuniamini Mkuu,kama Ulivyoonyesha Hapo Mapema,
Kwamba We Hujui Huaweni Ina Deal Na ELECTRONIC&TELECOMMUNICATIONS
( IT,SC,ICT) Etc,
Na Hizo Ndio Backbornes Za Operations Za Huawei,
Baada Ya Ban Saizi Wameingia Hadi Kwenye Agritech,yaani Wanashift Kutoka Kutegemea Bznes Zilizo Na Migogoro.
SOFTWARE Yao Tu Ya Harmony OS Ni Imefeli Kuingia Soko La Kimataifa Sasa Ww Endelea Kuwatetea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…