China yahimiza maendeleo ya matumizi ya Akili Bandia barani Afrika

China yahimiza maendeleo ya matumizi ya Akili Bandia barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,242
Reaction score
1,212
VCG41N1191384606.jpg


Katika miaka ya hivi karibuni uwekezaji wa China katika miundombinu ya kidijitali, vituo vya data na nishati umekuwa ukiongezeka kwa kasi katika nchi mbalimbali duniani. Wakati maendeleo ya matumizi ya akili bandia duniani yakipiga hatua na kufika kwenye miji ya Afrika, huku China ikiibuka kuwa nchi yenye mchango mkubwa katika kuendeleza miundombinu ya kidijitali, miundo ya Akili Bandia (AI), na nishati inayohitajika kuiwezesha miundo hiyo.



Moja ya maeneo yenye maendeleo ya kasi barani Afrika ni eneo la miundombinu ya mawasiliano ya habari. Kwenye maendeleo haya, bila shaka China imekuwa ni nguvu muhimu katika kufanikisha hatua mbalimbali zilizopigwa kwenye maendeleo hayo. Iwe ni kupitia uuzaji wa bidhaa za kidigitali kama simu mkononi, vishikwambi na kompyuta zinazotengenezwa China, hadi ujenzi wa mtandao mkubwa wa Mkonga wa mawasiliano (optic fibre) uliojengwa na makampuni ya China, na uwekezaji wa China kwenye ujenzi wa viwanda vinavyozalisha vifaa vya kidigitali barani Afrika kama vile simu za mkononi, ni wazi kuwa msingi wa maendeleo ya kidigitali katika nchi mbalimbali za Afrika unajengwa kwa kasi.



Pole pole kutokana na kuwa vituo vya Tehama na idadi ya vijana wenye ujuzi wa teknolojia hizo, Afrika pia imekuwa inapiga hatua kwenye kuendeleza sekta ya Akili Bandia. Kwa sasa kampuni ya Tehama ya China Huawei imejenga vituo kadhaa barani Afrika, na pia ina programu za mafunzo na mipango ya kuwaendeleza watu wenye vipaji vya teknolojia za kidigitali barani Afrika. Kuna jumla ya vituo saba vikiwa nchini Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Kenya, Morocco, Nigeria, na Afrika Kusini, kampuni hiyo pia inafadhili programu za mafunzo katika bara zima, na kila mwaka inatoa mafunzo kwa wanafunzi 12,000 wa Afrika kila mwaka.



Kampuni nyingine kubwa za teknolojia za China kama vile Alibaba zinapanua uwepo wao barani Afrika, zikitoa huduma za wingu na kuwekeza katika vituo vya data katika bara zima la Afrika. Kampuni ya Huawei imetangaza mipango ya kuwekeza $430m katika vituo vya data barani Afrika, na kampuni ya Alibaba tayari inatoa huduma za wingu nchini Afrika Kusini. Kutokana na kuwa teknolojia ya Akili Bandia na Tehama kwa ujumla inahitaji uwepo endelevu wa nishati, hadi kufikia mwaka jana, China ilikuwa imepata uwekezaji katika nchi 15 za Afrika ili kutoa nishati mara 10 zaidi ya nishati ya sasa.



Hata hivyo licha ya juhudi zinaendelea kufanywa na pande mbili za China na Afrika, bado kuna changamoto nyingi kwenye kufikia maendeleo zaidi kwenye matumizi ya teknolojia za akili bandia. Kwa sasa watu wengi wa Afrika wana simu za mkononi na vishikwambi, lakini matumizi yao yamejikita zaidi kwenye mawasiliano na burudani, na sio uvumbuzi, biashara au elimu. Na baadhi ya wanasiasa wa nchi za Afrika wana hofu na mwelekeo unaoonesha kuwa matumizi ya simu za mkononi na Internet vinasababisha ushawishi mkubwa kwenye mambo ya kisiasa na hata kuchochea ukiukaji wa maadili.



Baadhi ya watunga sera wa nchi za Afrika wanaona uwekezaji huo una hatari na faida. Hatari inaonekana zaidi kwenye uwezekano wa watu wenye hila wamiliki wa njia za vyombo vya habari vya kidigitali na wale wenye ujuzi wa akili bandia, wanaweza kufanya hila na kuelekeza maoni ya umma kwa mwelekeo wanaotaka, unaoweza kuwa na madhara kwa jamii, na hata kuchochea migongano kwenye jamii.



Hata hivyo hatari na faida za teknolojia za kidigitali na akili bandia zikiwekwa kwenye mizani, inaonekana kuna faida nyingi kuliko hatari. Hali hii inazitaka serikali za nchi za Afrika, kujenga na kuimarisha uwezo wa ndani, kuhimiza elimu na kupata ujuzi wa kutosha kudhibiti teknolojia hizo.
 
Back
Top Bottom