China yafunga makampuni ya Korea Kaskazini

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,566
Reaction score
8,325
China imeyaambia makampuni ya Korea Kaskazini yaliyo nchini mwake kufunga, wakati inajaribu kutekeleza vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya taifa hilo.
Makampuni hayo yatafungwa ifikapo mwezi Januari. Pia makampuni yanayomilikiwa na nchi hizo mbili yatalazimika kufunga.
China ambayo ni mshirika pekee mkuu wa Korea Kaskazini tayari imepiga marufuku biashara ya nguo na kupunguza bidhaa za mafuta.
Hatua hiyo ni sehemu ya hatua za kimataifa kujibu jaribio la sita na lenye nguvu la nyuklia
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambapo China ni mwanachama, lilipiga kura kwa wingi kuunga mkono vikwazo vipya tarehe 11 Septemba.
Wizara ya biashara nchini China ilisema kuwa imeweka siku ya mwisho ya siku 120 tangu kupitishwa kwa azimio hilo kwa kampuni yoyote ya Korea Kaskazini iliyo nchini China kufunga.
Korea Kaskazini imetengwa kisiasa na kiuchumi na sehemu kubwa ya biashara yake inafanya na China.
China tangu jadi imekuwa ikimtetea jirani wake huyo, lakini imemkashifu vikali kwa majaribio yake ya nyuklia na matamshi yake.
Mapema mwaka huu ilizuia kuingizwa kwa mkaa wa mawe kutoka Korea Kaskazini na bidha zingine.
Baada ya marufuku ya bidhaa za nguo, Korea Kaskazini imepoteza mapato yake kadha ya pesa za kigeni.

China imekuwa ikishinizwa kuchukua hatua kutoka kwa rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ameipongeza na mara nyingine kupinga sera za China.
Trump pia amehusika kwenye vita vya maneno na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, akimtaja kama "mtu wa makombora" aliye kwenye mikakati ya kujitia kitanzi.
Alisema kuwa hana lingine ila kuiharibu kabisa Korea Kaskazini ikiwa atalazimika kuilinda Marekani na washirika wake.
 
[emoji15] [emoji15] kuiteketeza Korea kaskazini yote ikibidi kufanya hivyo ili kuilinda marekani kama ataona inafaa...dah[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] ngoja nikapate staftahi kidogo ntarudi
 
Hapa ambacho huwa kinafanyika ni unafiki tu wa China na Russia hawa ni mabingwa wa uongo likija suala la vikwazo dhidi ya N Korea huwa wanaunga mkono azimio ila nyuma ya pazia biashara kila kitu kinaendelea kama kawaida huyu mchina anamuongopea tu Usa kama kumridhisha ila ukweli ni kwamba hawezi kumtenga mdogo wake kumtenga ni kulikaribisha shetani mlangoni kwa sababu usa akiipiga N Korea na akaikalia si ndiyo atakuwa milango mwa maadui zake China na Russia kitu ambacho hakitakiwi iwe kwa gharama yoyote ni jambo la muda tu ila ukweli ni kwa China na Russia wataendelea kumlinda kijana wao iwe masika iwe jua
 
china hataki usa aingie nkorea na ndio maana anafanya kila analo ona linafaa ili tu trump asipeleke watu wake pale kati
 
Hapa ambacho huwa kinafanyika ni unafiki tu wa China na Russia hawa ni mabingwa wa uongo likija suala la vikwazo dhidi ya N Korea huwa wanaunga mkono azimio ila nyuma ya pazia biashara kila kitu kinaendelea kama kawaida huyu mchina anamuongopea tu Usa kama kumridhisha ila ukweli ni kwamba hawezi kumtenga mdogo wake kumtenga ni kulikaribisha shetani mlangoni kwa sababu usa akiipiga N Korea na akaikalia si ndiyo atakuwa milango mwa maadui zake China na Russia kitu ambacho hakitakiwi iwe kwa gharama yoyote ni jambo la muda tu ila ukweli ni kwa China na Russia wataendelea kumlinda kijana wao iwe masika iwe jua

we unawaza kwa matege, china inabidi iheshimu maazimio ya umoja ili, kwanza isivuruge biashara zake na US, pili ili kumlidhisha trump asiivamie n.korea kitu kitakachopelekea US kukaa mlangoni mwa china
 
Linapokuja suala la kuilinda Marekani na washirika wake, Trump has no any other option but to "completely destroy" NK. Nawaonea huruma sana wananchi mafukara wa NK wasiojua hili wa lile zaidi ya kutawaliwa kama punda na yule dhalimu. Mwenyezi Mungu wahurumie.
 
Hapa ambacho huwa kinafanyika ni unafiki tu wa China na Russia hawa ni mabingwa wa uongo likija suala la vikwazo dhidi ya N Korea huwa wanaunga mkono azimio ila nyuma ya pazia biashara kila kitu kinaendelea kama kawaida huyu mchina anamuongopea tu Usa kama kumridhisha ila ukweli ni kwamba hawezi kumtenga mdogo wake kumtenga ni kulikaribisha shetani mlangoni kwa sababu usa akiipiga N Korea na akaikalia si ndiyo atakuwa milango mwa maadui zake China na Russia kitu ambacho hakitakiwi iwe kwa gharama yoyote ni jambo la muda tu ila ukweli ni kwa China na Russia wataendelea kumlinda kijana wao iwe masika iwe jua
Sio rahisi namna hio....jua watj wako under Big Screen Suveillance
 
Back
Top Bottom