China watumia Blockchain kufuga kuku

China watumia Blockchain kufuga kuku

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,312
Reaction score
12,198
p-1-in-china-you-can-track-chicken-on-the-blockchain.jpg

Nchini china wametengeneza mfumo wa ufatiliaji maendeleo ya kuku kupitia blockchain. Mfumo utasaidia wateja kutouziwa kuku waliokufa au waliokwisha muda wao wa kukaa sokoni na badala yake mnunuzi ataweza kujua toka kuku alipototolewa, alipochinjwa mpaka atakapokua dukani tayari kuuzwa.
“All info related to the chicken can be verified in the blockchain,” says Xuefeng Li, CTO of ZhongAn Technology, the tech incubator of the Chinese insurance company ZhongAn, which developed the technology.
Baadhi ya taarifa zitakazopatikana ni pamoja na umri wa kuku, eneo alilototolewa, umbali aliotembea kwa kila siku, kiwango cha uchafuzi wa hewa alichopata, kiwango cha maji alichokunywa, siku aliyochinjwa.
Vyote hivi utavipata kupitia blockchain kwa kutumia Gogochicken system ambapo taarifa hizi hutumwa kutoka kifaa anachokua kafungwa kuku mguuni muda wote.
Jinsi gani wenzetu wametuacha mbali katika kuziona fursa!..
In China, You Can Track Your Chicken On–You Guessed It–The Blockchain
 
Hongera zao.

Sisi uku ni mwendo wa vibudu na mizoga.
 
Hahaha sisi tunajenga viwanda kwanza, unataka kutupoteza na ufugaji wa kuku huo.
Tanzania ya viwanda, sio Tanzania ya kuku.
 
Hii itawakomboa wanaume wa dar maana wana kula kuku kinda ...wengine vibudu
 
Hahaha sisi tunajenga viwanda kwanza, unataka kutupoteza na ufugaji wa kuku huo.
Tanzania ya viwanda, sio Tanzania ya kuku.
yaani ninyi ndo wapinga kila kituuu huwa hatuelewi hata mnataka nini
 
yaani ninyi ndo wapinga kila kituuu huwa hatuelewi hata mnataka nini
Hahaha ndugu, kufuga hata kienyeji sisi hatuwezi, hatupingi tunajijua sisi wadanganyika huo ndio ukweli.
Hahaha sasa hapo tumepinga nini?! Mlitaka nanyie mfuge tukakataa?! Nyie huwa mnatekeleza ILANI, kwani ufugaji huo wakuku huko kwenye ILANI?! Hahaha tekelezeni kama mnaweza ndugu hamjashikwa mikono na wapingaji.
 
mkuu siasa ni sehemu ya maisha usifanye kama ugonvi. mimi mwenyewe ni CHADEMA Ila wa dr Slaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom