China:Tutaondoa tatizo la umeme venezuela

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,368
18,919
China: Tutaondoa matatizo ya kukatwa mtandao wa umeme nchini Venezuela
Mar 14, 2019 02:30 UTC
Serikali ya China imesema kuwa, ipo tayari kusaidia kuondoa mtatizo ya kukatwa mtandao wa umeme nchini Venezuela.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lu Kang sambamba na kuonyesha wasi wasi juu ya kuendelea giza nchini Venezuela, imeonyesha matumaini kwamba pande husika nchini humo zitaweza kubaini haraka chanzo cha kukatwa umeme na kuurejesha katika hali ya kawaida.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari na mashuhuda, Jumanne ya jana baadhi ya maeneo ya Venezuela yalirejea katika hali yake ya kawaida, huku maeneo ya baadhi ya viunga vya mji mkuu na viunga vya maeneo ya magharibi karibu na mpaka wa Colombia, bado yameendelea kusalia gizani kutokana na kukatika umeme.
Kukatika umeme nchini humo kulianza Alkhamisi iliyopita. Hii ni katika hali ambayo Rais Nicolás Maduro wa Venezuela ameituhumu Marekani kwa kuibuka kasoro katika mitambo ya kuzalisha umeme ya 'Hydroelectric' kupitia mashambulizi ya njia za mtandao.
Kufuatia hali hiyo, maeneo muhimu kama vile hospitali, taasisi za mafuta, zimekumbwa na matatizo makubwa ikiwemo kufungwa shule na baadhi ya ofisi za serikali. Aidha idara za kuhifadhi vyakula nazo zimekumbwa na matatizo ikiwemo kuharibika vyakula hivyo.
 
Back
Top Bottom