China(PRC) na Taiwan(ROC) bado wapo kwenye civil war

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,243
12,772
Kabla ya vita ya pili ya Dunia, China ilikuwa ikiongozwa chama cha Wakoumitang. Wakiita nchi yao Republic of China. Hawa walikuwa chini ya Kai Shek. Wakoumitang walifanya kazi kubwa sana kuiunganisha China. Wakikomesha wababe wa kivita vurugu zingine. Lakini wakatokea wapinzani wao. Wacommunist chini ya Mao.

Hivyo China ikaingia kwenye civil war. Wakati na karibu na WWII Japan ikaivamia China. Serikali ya wakoumitang ilipigana sana vita dhidi ya wajapan. Huku wacommunist wakiendelea kukua na sometimes wakipgana vita kuzidi kuwadhoofisha wakoumitang. Japo na kwa namna walishiriki kupigana na wajapan.

Baada ya Japan kushindwa vita ya pili ya dunia, wacommunist wa Mao wakaibuka wakiwa na nguvu sana, huku wakoumitang wakiwa hoi kabisa. Basi kwenye muendelezo wa civil war yao, wakoumitang wakashindwa na kukimbilia kisiwa cha Taiwan. Wasomi, matajiri wakakimbia na mali nyingi kwenda Taiwan. Huku nyuma wacommunist wakaunda serikali yao, People republic of China(PRC). Wale waliokimbilia Taiwan wakiendelea kujiita(ROC) na wakidai kuwa wao ndiyo wenye kutawala China yote. Na sehemu ya mpango wao ilikuwa ni kurudi tena kutawala China yote.

Mwanzoni hata UN iliitambuq serikali iliyopo Taiwan kama serikali halali ya China yote. Lakini baadaye wakabadilika, wakiitambua serikali iliyo China bara kama serikali ya China yote.
So huu mgogoro ni muendelezo tu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hakuna hero wala villain.
 
Kwa mtazamo wangu nilipoisoma Historia niliamua kuwa upande wa Chang Kai Shek, maana Mao na kundi lake walimwondoa kwa kutaka kuleta Ukomunisti, madai ya CHINA kuwa Taiwan ni yao, ni sawa tu na madai ya Taiwan ni kuwa China mainland ni yao.Hakuna mwenye haki dhidi ya mwenzie in real sense, ni watu wale wake, ambao hawakutaka Ukomunisti walikimbia Taiwan, sasa ni nani mwenye haki dhidi ya mwenzie.
 
Hata mimi namkubali zaidi Kai Shek. Na hata vijana wa sasa wa China wengi wameanza kumkubali Kai Shek. Maana alifanya kazi kubwa kuiunganisha China na kupambana na Wajapan. Lakini wataiwan wengi wanamchukia. Alivyoenda Taiwan akaanzisha martial law iliyowatesa sana.

Lakini mwisho wa siku, kati ya China Taipei na China Bara. Hakuna mwenye haki zaidi.
 
Republic Of China [ ROC ] chini ya chama cha kibepari cha Kuomitang chini ya Sun Yat Sen na baadae Chiang Kai sheki ilikuwa imeoza inanuka rushwa, sera mbovu za umiliki wa ardhi, ufisadi, Uongozi mbovu ndipo Mao Zedong akachukizwa na hiyo hali akaanza kujifunza falsafa za kijamaa kupitia vitabu na magazeti yaliyokuwa yanaandika habari kuhusu nchi ya kijamaa ya Urusi chini ya Lenin ndipo Mao akajikusanya na wenzake Kumi akiwemo Zhuo Enlai na kuanzisha Chama cha kijamaa kwenye boti 1921 ili kuja kuleta ukombozi wa hayo matatizo yanayo sababishwa na chama Cha kibepari cha Kuomitang hasa hasa tatizo la umiliki wa ardhi kwa wakulima . Mao alitembea vijiji kwa vijiji kwa miguu kuwaeleza wachina dhima nzima ya kijamaa ambavyo itaweza kuwasaidia kukomesha matatizo yao chini ya serikali dhalimu ya kibepari ya Kuomitang.wachina waliowengi wakaanza kuamini falasa za kijamaa za Mao[ Maoism] na kuanza kujiunga na chama Cha kikomunisti Cha China [ CPC ] kwa ajili ya kupinga serikali ya Kuomitang . Wachina waliowengi wengi na kwa wingi waliongezeka katika kujiunga na CPC na kuunga juhudi za mapambano huku China ikiwa imepasuka vipande viwili vya kifalsafa ujamaa wale waliokuwa wanaunga juhudi za CPC na wanachama wa CPC na kipande kingine wale waliokuwa wanaunga mkono sera za kibepari za Kuomitang . Mnamo mwaka 1927 wanachama wa CPC wakaanzisha jeshi lao kwa ajili ya ukombozi waliolipachika jina la People's Liberation Army [ PLA ] kwa ajili ya kuitoa madarakani Kuomitang .
 
Kwa mtazamo wangu nilipoisoma Historia niliamua kuwa upande wa Chang Kai Shek, maana Mao na kundi lake walimwondoa kwa kutaka kuleta Ukomunisti, madai ya CHINA kuwa Taiwan ni yao, ni sawa tu na madai ya Taiwan ni kuwa China mainland ni yao.Hakuna mwenye haki dhidi ya mwenzie in real sense, ni watu wale wake, ambao hawakutaka Ukomunisti walikimbia Taiwan, sasa ni nani mwenye haki dhidi ya mwenzie.
Kwa maelezo haya ya mtoa mada, Taiwan iachwe kama ilivyo bila kuingiliwa na China.
 
Aleyn: China na Taiwan ni nchi moja, lakini kisiasa walichukua nji tofauti, upande wa utawala wa zamani, yaani wa Chang Kai Shek,waliamua kumpisha Mao mainland China na kwenda Taiwan. Ungekua labda ulifanyika uchaguzi na kundi moja likashinda angalau upande ulioshinda ninge sympathize nao, Mao aliingia kwa nguvu,Wachina hawakushirikishwa kuwa wanataka Ukomunisti, ambao hawautaki wakaenda Taiwan,sasa nani mwenye haki dhidi ya mwenzie.Na hata ukifanya referendum leo,watu wa Mainland China wataitaka Taiwan, na watu wa Taiwan hawataitaka Mainland China.Ndio maana kwa upande claims za China zinaweza kuwa pia za Taiwan.
 
Yani maana yake mwenye nguvu ndio mwenye haki..
Maundu: Usingetegemea philosophia toka kwa China, maana yeye anailaumu Marekani kwa kuwa kama mwenye nguvu ndio mwenye haki, na yeye anafanya kitu hicho hicho kwa Taiwan.China akiwa a single super power atafanya yale yale anayolaumiwa Marekani, na hata Urusi pia, anachokifanya Ukraine ni philosophic ile ile mwenye nguvu mpishe.
 
Back
Top Bottom