China: Je ndio nchi inayoongoza kwa werevu duniani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

China: Je ndio nchi inayoongoza kwa werevu duniani?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Viper, May 9, 2012.

 1. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Matokeo ya china katika mitihani ya kimataifa shuleni, ambayo haijawahi kuchapishwa, ni ya kuridhisha saana. Hii ni kauli ya Andreas Schleicher, ambaye anahusika na mitihani ya kimataifa ya Pisa.
  [​IMG]
  Mitihani hii hufanywa baada ya kila miaka mitatu na kuandaliwa na shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo. Lengo lake huwa ni kuchunguza uwezo wa mtoto kusoma, kufanya hesabu na sayansi.

  Mitihani ya Pisa, imetumika kama kigezo cha kimataifa kwa wanafunzi kote duniani. Matokeo haya yanaonyesha kuwa China ina mfumo wa elimu ambao unapiku nchi za magharibi.

  Licha ya wengi kupiga darubini sana hali ya kiuchumi na kisiasa nchini China, ripoti hii inatoa fursa kwa watu kuona nchi hiyo inavyoelimisha kizazi kijacho. Wanajizatiti sana.

  Mitihani ya Pisa mwaka 2009, ilionyesha wazi kuwa Shanghai ilikuwa juu kwenye orodha ya waliofanya vyema kielimu kimataifa.

  Hata hivyo haikuwa wazi ikiwa Shanghai pamoja Hong Kong ambayo pia ilifanya vizuri sana, ziliwakilisha ipasavyo kikanda au kulikuwa na maeneo mengine ambayo yalifanya vizuri zaidi.

  Bwana Schleicher anasema kuwa matokeo ambayo hajachapishwa yanaonyesha kwa wanafunzi katika maeneo mengine ya China pia wanafanya vyema sana.

  [​IMG]
  Hata katika maeneo ya vijijini na maeneo yaliyotengwa kiuchumi, ni wazi kuwa wanafunzi wana bidii sana" alisema Schleicher.

  Aliongeza kuwa matokeo ya mitihani yanaonyesha wanafunzi wanajizatiti sana kuweza kufanikiwa licha ya mazingira magumu sawa na pengo lililoko kati ya wanafunzi kutoka familia maskini na zile tajiri.


  Bwana Schleicher alielezea kushangazwa zaidi na matokeo ya shule za vijijini ikilinganishwa na alichoshuhudia mijini kama vile Shanghai. Yaani hali wanavyojizatiti wanafunzi ni ya kutia moyo.


  Nchini China msingi wa maisha bora ni elimu, na kulingana na utafiti huo hilo lilibainika wazi kwani wanafunzi wanaelewa kuwa bila elimu, maisha yako hayatakuwa mazuri.


  Matokeo ya wanafunzi wanaotoka famailia zisizojiweza nchini China, bila shaka inaweza kuonewa wivu na nchi za magharibi kulingana na bwana Schleicher.


  Katika juhudi zake kupata picha halisi, mitihani ilifanywa katika mikoa tisa ikiwemo katika maeneo yenye viwango vya juu vya umaskini, katika maeneo yenye kipato cha kadri na mwishowe katika maeneo yenye matajiri wengi.


  Wanafunzi wa shule ya upili ya Nanjing wanafahamu vyema kauli mbiu yao " lazima niende katika chuo kikuu" walisika wakisema nje ya shule yao.


  Hata hivyo serikali ya China imekataa kuruhusu kuchapishwa kwa matokeo ya mitihani hiyo. Lakini bwana Schleicher anasema kuwa matokeo hayo yanaonyesha picha halisi ya jamii kuekeza kwa ujumla katika elimu  [​IMG]

  Katika ziara yake katika mkoa mmoja, bwana Schleicher anasema aliona majengo ya shule yakiwa yanapendeza sana.
  Katika nchi za magharibi, ungedhani majengo hayo ni maduka ya kifahari.


  Pia kulikuwa na tofauti kubwa kati ya wanafunzi vijana, walioulizwa kwa nini wanadhani wanafunzi wanafaulu sana shuleni.
  Raia kutoka Marekani husema ni bahati tu , ni mtu kuzaliwa akiwa ana akili ya kujua mfano hesabu na ikiwa hiyo nidio maoni ya wengi wanafunzi huonelea ni bora kufanya anachoona anaweza mwenyewe.


  Barani Ulaya elimu ni juu ya urithi, mfano wanafunzi husema babangu alikuwa seremala kwa hivyo na mimi nitakuwa seremala, haoni haja ya kufanya bidii kusoma.Nchini China wanafunzi wengi husema inategemea bidii yangu, ikiwa nitafanya bidii bila shaka nitafanikiwa masiahani.

  SORCE - BBC BBC Swahili - Kwa Kina - China: Je ndio nchi inayoongoza kwa werevu duniani?


   
 2. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Hebu waone hapa wanajiandaa na paper huku wamewekewa drip, hakuna kulala!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Sashel

  Sashel JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Viper ni kweli hawa wenzetu ni werevu na wana bidii sana, na hii yote naamini ni kutokana na malezi yao toka wakiwa wadogo wanakuzwa katika utaratibu ambao wengine wanaweza kuuona ni harsh (hasa western countries). Kuna mwana-mnama mmoja (mchina) ni Prof wa Yale University, yeye ameandika kitabu kinaitwa 'BATTLE HYMN OF THE TIGER MOTHER' ameelezea tofauti na mgongano wa tamaduni na malezi kati ya westerns na chinese na jinsi wamama wa kichina wanavyolea watoto wao vizuri hata kuwa na mafanikio makubwa katika maisha yao.

  hapa naweka kipande tu cha sehemu ya maelezo yake:

  Part One
  The Tiger, the living symbol of strength and power, generally inspires fear and respect.

  The Chinese Mother
  A lot of people wonder how Chinese parents raise such stereotypically successful kids. They wonder what these parents do to produce so many math whizzes and music prodigies, what it's like inside the family, and whether they could do it too. Well, I can tell them, because I've done it. Here are some things my daughters, Sophia and Louisa, were never allowed to do:
  - attend a sleepover
  - have a playdate
  - be in a school play
  - complain about not being in a school play
  - watch TV or play computer games
  - choose their own extracurricular activities
  - get any grade less than an A
  - not be the #1 student in every subject except gym and drama
  - play any instrument other than the piano or violin
  - not play the piano or violin....

  the Chinese mother believes that (1) schoolwork always comes first; (2) an A-minus is a bad grade; (3) your children must be two years ahead of their classmates in math; (4) you must never compliment your children in public; (5) if your child ever disagrees with a teacher or coach, you must always take the side of the teacher or coach; (6) the only activities your children should be permitted to do are those in which they can eventually win a medal; and (7) that medal must be gold.

  Haya wamama wa Tz- mnataka watoto wawe "vichwa" inabidi kuingia kazini, I would recommend the book for all mothers our there- raising-up kids is no leisure.

  NB: hapa amezungumziwa mama zaidi maana ndiye mlezi aliye karibu sana na mtoto, hivyo hata baba anaweza fanya hivyo pia
   
Loading...