Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,662
Asante leo usiku nayaamsha madude mengine kuanzia saa 4MJUKUU WA CHIFU hili jukwaa umekodi nini? naona threads zako tu aisee. hongera
Poa mkuu
Hao WAZARAMO (wahamiaji), walipofika hayo maeneo hawakuwakuta wenyeji? Na hao wenyeji ni kabila gani?Hili ni moja ya kabila ambalo linapatikana hapa hapa Tanzania hasa upande wa mashariki.
Japo habari na historia la kabila hili zilishaandikwa, hasa juu ya asili ya neno Uzaramo au Wazaramo. Kwa kuwakumbusha tu, Wazaramo maana yake ni waamiaji. Naweza kusema kuwa, kwa mujibu wa wataalamu walioandika habari za makabila ya tanzania na Afrika kwa ujumla , wanasema kuwa, Wazaramo ni jumla ya koo mbalimbali zilizofika Pwani ya Afrika mshariki, hasa maeneo ya mwambao wa Dar es salaam hata kabla ya miaka ya 1600.
Koo hizo ambazo zilitokea bara zilikuja Kuzarama yaani kuhamia maeneo ya Pwani kwa lengo la kufanya shughuli mbalimbali za kibaishara na uvuvi kwenye meneo hayo. Ukweli ni kwamba neno Kuzarama ni la kibantu na maana yake ni Kuhamia.
Hivyo mtu anayehamia huitwa Mzaramo na wakiwa wengi wanaitwa Wazaramo. Na wakati wageni hao wanafika pwani, waliuliza nyinyi ni wakina nani na ndipo wenyeji hao walipojibu kuwa wao ni Wazaramo, yaani wahamiaj. Basi kuanzia hapo yaani miaka ya 1840/1850 kipindi wageni wanafika na kuandika habari za waafrika Watu waliofika Pwani walifahamika kama Wazaramo.
Jambo la kufahamu hapo ni kwamba, koo zilizokuja kuzarama ni kutoka maeneo mbalimbali. Hivyo kuna uwezekano wa kuwa , koo za makabila mengi ziliunda kabila hili la kizaramo. Na ndio maana tamaduni nyingi za kizaramo zipo kwenye makabila mengi japo kuna utofauti kidogo ambao ulisababishwa na masuala ya kijiografia.
Mara baada ya kufahamu habari hizo, tupate kufahamu chimbuko au mahali ambapo kabila hili la kizaramo zilianzia. Inafafanuliwa kuwa, kabila la wazaramo lilipata kuchimbukia maeneo ya Moneromango au wengi hutamka Mwanarumango.
Hama kuhusu Maneromango, ni sehemu inayopatika katika wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani. Inafafanuliwa kuwa eneo hili ndio chimbuko la Wazaramo kwa kuwa, kiongozi wa kabila hili Bwana Pazi Kilama alipata kuishi maeneo hayo, na hata mpaka vita kati ya Wazaramo na Wakamba vinatokea, vilipiganiwa maeneo haya.
Hata koo za Kibena kwa mara ya Kwanza walikutana hapo na Wazaramo na kuachana maeneo ya Moneromango. Na zaidi ya hapo, hata zile koo maarufu kama ukoo wa wakina Samatha na ukoo wakina Kawambwa, zilipata kuishi maeneo ya Monerumano au Mwanarumango.
Na pia kulikuwa na habari nyingi za kuvamiwa na simba, inasimuliwa kuwa maeneo hayo ndio yalikuwa maeneo ambayo yalikuwa yakivamiwa sana na simba. Hivyo maeneo ya Monerumango ndio moja ya maeneo ya mwanzo kukaliwa na Wazaramo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba unitag ukipata jibuHao WAZARAMO (wahamiaji), walipofika hayo maeneo hawakuwakuta wenyeji? Na hao wenyeji ni kabila gani?
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mleta mada....kulikuwa na habari nyingi za kuvamiwa na simba, inasimuliwa kuwa maeneo hayo ndio yalikuwa maeneo ambayo yalikuwa yakivamiwa sana na simba. Hivyo maeneo ya Monerumango ndio moja ya maeneo ya mwanzo kukaliwa na Wazaramo
Sema wachoyo sana wa lugha hawataki kuwafundisha wageni lugha yao!Wazaramo...wapo wanaokizungumza hadi sasa
Niliposikia wahamiaji kutoka bara...nikajua ni bara kweli...wapi..mleta mada anasema wanatokea Kisarawe! Sasa Kisarawe toka lini ikawa Bara. Nina wasiwasi mleta mada ni mzaramo tena mjukuu wa Chifu Pazi (nimemkumbuka Idd Pazi, golikipa matata sana enzi hizo...mpira tunaufuatilia 'Redio Tanzania-Dar es-Salaam'..watangazaji Omary Jongo na Ahamed Jongo na dereva wa OB van nimemsahau jina). Wazaramo kwa 'kukuza mambo hawajambo'. Eti wahamiaji kutoka bara. Ha ha haaa!Wazaramo hawanaga chimbuko
Mkuu mimi nimefahamu kwamba amesema Manerumango inapatikana Wilaya ya Kisarawe. Au sikumuelewa sawasawa?Niliposikia wahamiaji kutoka bara...nikajua ni bara kweli...wapi..mleta mada anasema wanatokea Kisarawe! Sasa Kisarawe toka lini ikawa Bara. Nina wasiwasi mleta mada ni mzaramo tena mjukuu wa Chifu Pazi (nimemkumbuka Idd Pazi, golikipa matata sana enzi hizo...mpira tunaufuatilia 'Redio Tanzania-Dar es-Salaam'..watangazaji Omary Jongo na Ahamed Jongo na dereva wa OB van nimemsahau jina). Wazaramo kwa 'kukuza mambo hawajambo'. Eti wahamiaji kutoka bara. Ha ha haaa!
Zamani pwani zote za Africa ziliogopwa waafrica kuweka makazi, hawakuishi watu, sababu kubwa ni kuwa waliogopa kukamatwa na kuuzwa utumwani kirahisi. wachache walowahi pata ishi ni wale watumwa walio choka kuendelea na misafara kwa sababu mbalimbali km kuugua. Afya mbovu, kuvuja damu sana, walitelekezwa maeneo ya pwani, hata ukiugua watakwambia jikaze ufike pwani km wakikupenda! wasipokupenda wanakuulia kwa mbali! hkna kesi unakuwa chakula cha Mbweha, fisi! nkHao WAZARAMO (wahamiaji), walipofika hayo maeneo hawakuwakuta wenyeji? Na hao wenyeji ni kabila gani?
Sent using Jamii Forums mobile app
Zamani pwani zote za Africa ziliogopwa waafrica kuweka makazi, hawakuishi watu, sababu kubwa ni kuwa waliogopa kukamatwa na kuuzwa utumwani kirahisi. wachache walowahi pata ishi ni wale watumwa walio choka kuendelea na misafara kwa sababu mbalimbali km kuugua. Afya mbovu, kuvuja damu sana, walitelekezwa maeneo ya pwani, hata ukiugua watakwambia jikaze ufike pwani km wakikupenda! wasipokupenda wanakuulia kwa mbali! hkna kesi unakuwa chakula cha Mbweha, fisi! nkHao WAZARAMO (wahamiaji), walipofika hayo maeneo hawakuwakuta wenyeji? Na hao wenyeji ni kabila gani?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kitaalamu; Coastal zones as including the Land Area of within 60 Km of adjacent near shore waters, well inaweza kuwa hata zaidi but still ni pwani! kule kwao Musoma wanaita Mwibara.Kangi Lugora ndo mbunge! ilikuwa ni sehemu ya Ukerewe baadaye wakabadili ikaitwa Kibara. hii ina apply kotekote Bahari na Ziwa.Wazaramo ni waluguru waliohamia Pwani kwenda kupigana vita, wakaungana na wandengereko. Kzaramo na kiluguru ni kitu kimoja.
Ukisema walitokea Bara unakuwa haupo specific kwa sababu watu waliotokea bara na kuja Pwani ni waswahili. Wazaramo siyo waswahili.
Labda ni kutoelewana.Kitaalamu; Coastal zones as including the Land Area of within 60 Km of adjacent near shore waters, well inaweza kuwa hata zaidi but still ni pwani! kule kwao Musoma wanaita Mwibara.Kangi Lugora ndo mbunge! ilikuwa ni sehemu ya Ukerewe baadaye wakabadili ikaitwa Kibara. hii ina apply kotekote Bahari na Ziwa.
Moro/ main land to Dar /coastal area = Land area within ni 178 Km, kwa umbali huu Bado ni specific reasonable distance ya kuwa Bara, kumbuka Sultani alitawala visiwani na kuongezea Km 25 kutoka pwani ya EA. kutoka pwani ya Msumbiji mpaka Lamu. if my memory serve me well!!!! kwa hiyo Urugulu kwenda ndani zaidi bado ni Bara tu!
kiswahili (Wabantu)ndiyo Lugha ya Biashara iliyotumika kwa mawasiliano Bara na Pwani, kiswahili chenye lafudhi yenye radha safi iko ukanda wa pwani ya EA Mombasa, Tanga, Wazaramo, Wakwere, nk!
Kiswahili ni Kibantu, -Nilotics siyo wabantu, ukisema Wazaramo siyo Waswahili, ina maana Zaramo people siyo wabantu, hapa si kweli hata kidogo!!. Au prove!!!! Rejea ''wimbo wa shabani Madobe''