Chimbuko la msemo 'witch hunt'

Chimbuko la msemo 'witch hunt'

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
7,849
Reaction score
8,728
CHIMBUKO LA MSEMO 'WITCH HUNT'!

KSM-WP-04.jpg

Kwenye simulizi pendwa, zilipendwa, za hadithi ya 'MASHIMO YA MFALME SULEIMAN' kuna 'character' mmoja mashuhuri sana naye si mwingine bali ni 'kibibi kizee kichawi Gagula' kilichokuwa kishauri kikuu cha mfalme mkatili wa wakukuana aliyeitwa Twala. Mara kwa mara, kwa ushauri wa kizee Gagula, mfalme Twala aliitisha ngoma ya kutambua wachawi ambapo yeye kizee Gagula alikuwa anapagawa na pepo linalomuelekeza wachawi na watu wenye nia mbaya na mfalme.
Kwenye ngoma ya kutambulisha wachawi kizee kichawi Gagula, pichani juu, kikimsonta mtu tu basi kikosi maalum cha wauaji humshambulia muhusika na mikuki na kumuua ndani ya sekunde chache. Kwakweli sijawahi kusoma kitu cha kuogofya kama ngoma ya kutambulisha wachawi ya kizee kichawi Gagula, lakini hiyo, ninavyofahamu ndiyo asili ya usemi mashuhuri wa 'WITCH HUNT'!

NB: 1) Katika Historia inasemekana pia kuwa mfalme Chaka wa wazulu naye alikuwa anaendesha ngoma au gwaride la kutambua wachawi na wabaya wake ambapo alikuwa anatumia kikundi cha wachawi kikiongozwa na kiranja wao ambaye alikuwa mkuu wa wachawi wa mfalme, ambaye alikuwa mwanamke!
2) Witch hunt zingine zilifanyika Ulaya ya enzi za giza na watuhumiwa wengi, wengi wao wakiwa wanawake, waliangamizwa kwa hasira ya umma!

c.c. mshana jr
 
Safi

Mkuu hii hapa mashimo ya mfalme Suleiman

Hadithi ya mashimo ya mfalme Sulemani - JamiiForums
 
Back
Top Bottom