Chimbuko la Freemasonry Khemet

Chimbuko la Freemasonry Khemet

Joined
Nov 7, 2019
Posts
36
Reaction score
75
CHIMBUKO LA FREEMASONRY KEMET.

Ujuzi ni nguvu, maarifa ni nguvu na yanawakilisha kiasi kilicho patikana cha kujifunza, ambacho wa Kemet wa kale walikuwa wamefikia katika uwezo wa kutumia kikamilifu nguvu ya ubunifu (creative force) iliyopo kwenye Tezi ya Penueli - jicho la tatu (hii ni miongoni mwa siri kubwa ya pili kuhusiana na fiziolojia ya binadamu, kwa kweli hili ni somo jingine katika muda na wakati mwingine) na iliwapa uwezo uwezo wa kuweza kutumia asilimia 95% ya uwezo wao wa akili kwamba iliwapa uwezo wa kutumia ubongo wao kwa asilimia 95% au nguvu ya ubongo.

Ubongo bado unabaki kuwa kitendawili kwa mtu wa magharibi na jambo hili (kuwa na nia ya kuamsha na kutumia kiasi kikubwa cha uwezo wa akili/ubongo bado haijawahi kutokea) halijarudiwa tangu wakati huo, na hili pekee(Pineal gland) ndilo lililo wabadilisha Wa-Kemet wa kale kuwa Miungu wakuu Duniani.

(Rejea: ERICK VON DANIKEN "Chariots of the Gods" yaani "Magari Ya Miungu"

Wajenzi wa Kemet hawakuwa Alien wa Angani (Space), bali walikuwa viumbe wa mwilini (mortal beings), watu, ambao hawawezi kutazamwa nje ya dhana ya Miungu Duniani.

Ujuzi wao wa kuweza kutambua Tezi penueli na kugundua nguvu iliyopo katika Tezi hiyo, iliwafanya waweze kutumia asilimia 95% ya ubongo wao na kutenda mambo makubwa yasiyo ya kawaida ikiwemo kujenga Kemet ya kale...walionekana kama Miungu wenye nguvu nyakati hizo (The Supreme Deities)

(Rejea: Cheikh Anta Diop: "Precolonial Black Africa" yaani Afrika Nyeusi Kabla Ya Ukoloni")

Hayo yalionekana kupitia nguvu yao ya Ubunifu (jicho la tatu) na uwezo wao wa kuvuka/kushinda fikra za Ulimwengu wa magharibi na kubadilika kabisa mpaka kuwa na maelewano mazuri kati yao na Dunia au Ulimwengu kwa ujumla (ilitazamwa kama Operative Mansonry na Speculative Maaonry)

Dhana ya "Kama ilivyo juu ndivyo ilivyo chini" mtu hawezi kuwepo bila mwingine: Tunatumia chini ya asilimia 10 ya uwezo wetu wa ubongo kwa sehemu, kwasababu tumefundishwa kumuamini huyo Mungu wa siri asiyeonekana ambaye hayupo/hajawahi kuwepo, Na tumekuwa tukimtegemea siku za hivi karibuni kwa zaidi ya miaka 450 atufanyie kile tunacho paswa kufanya wenyewe kwa ajili yetu.

(Maandiko haya na nakala hizi zimeundwa ili kuwafufua wale ambao walifanywa vipofu, viziwi na mabubu juu ya ujuzi wa nafsi zetu).

"IJUE NAFSI YAKO"

Know thyself

ITAENDELEA.
 

Attachments

  • FB_IMG_1754319269093.jpg
    FB_IMG_1754319269093.jpg
    69.2 KB · Views: 32

Similar Discussions

Back
Top Bottom