Chiluba v/s malkia

KIGENE

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,552
813
Wakati bado mpya mpya kwenye ikulu ya Lusaka nchini Zambia rais F Chiluba alipata fursa ya kumtembelea malkia wa Uingereza Elizabeth saa ya makulakula ikawadia meza imesheheni kila aina ya maanjumat Chiluba akagundua mke wake Vera bado kaushamba hakajamtoka nakuchanganua mpangilio wa mezani hawezi Kwa ujasiri wa ajabu akamwomba malkia amruhusu sala yakuombea chakula aiendeshe yeye kwa kilugha (kiwemba) baada ya kuruhusiwa akaanza"Mke wangu Vera kaa makini unisikilize kitambaa cheupe nichakujifunga chakula kisikudondokee kwenye nguo kijiko kikubwa kiasi ni kwa ajili ya supu hiyo uma unashika na mkono wa kushoto na kisu mkono wa kulia mambo mengine uwe unaniangalia ninavyofanya AMINA"
 
Ahahahahaaah!! Hapo lazima wapambe wake walistukia mchezo mzima!
 
Hapo hata Malkia akija kugundua anaweza akampa jamaa nishani ya Upendo....
Dah, so impressing.....
 
Hakutaka kuaibishwa lol! Kuna mwarabu alienda Zambia sasa wazambia wakiitana wanaanza na 'mamdalaa' sasa muarabu akawa anadhani wanaitwa Abdallah,aliporudi kwao akawasimulia wenzake nimeenda Zambia kila mtu anaitwa Abdallah majina mengine sijui hawayapendi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom