Chiligati hana sifa za uongozi - Diwani CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chiligati hana sifa za uongozi - Diwani CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Apr 27, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,060
  Trophy Points: 280
  DIWANI wa kata ya Mgama, wilayani Iringa Vijijini, Denis Lupala (CCM), yuko matatani baada ya kumwita Naibu Katibu Mkuu CCM, Tanzania Bara, Kapteni John Chiligati, kuwa ni fisadi na anapaswa kuvuliwa gamba kama Katibu Mkuu aliyepita Luteni Yusuf Makamba na wenzake.

  Diwani huyo anadaiwa kutoa kauli hiyo hivi karibuni mkoani Iringa wakati Chiligati na viongozi wengine wapya wa sekretarieti ya CCM taifa alipofanya ziara mkoani humo kwa ajili ya kujitambulisha.

  Diwani huyo ambaye tayari ameitwa na sekretarieti ya wilaya na Kamati ya Maadili kujadiliwa kwa utovu kwa Chiligati na viongozi wengine waandamizi wa CCM ambao alipendekeza watimuliwe.

  Akithibitisha kuitwa kwenye vikao hivyo, Lupala alisema alipewa barua ya kuitwa kuhusu tuhuma hizo, lakini hakuhojiwa.

  ‘Kweli waliniita na mwanzoni niliambiwa kikao kitanijadili kwa utovu wa nidhamu niliouonyesha badala yake tulijadili tukio la jukwaa kuanguka wakati Chiligati akihutubia," alisema diwani huyo.

  Hata hivyo alijigamba kuwa alikuwa amejiandaa kupangua hoja zao kwani hadi sasa binafsi hataki Chiligati abaki kwenye nafasi hiyo kwa madai kuwa anapaswa kuvuliwa gamba kama viongozi wenzake aliokuwa nao kwenye sekretarieti iliyopita.

  "Nilijipanga vizuri kuwajibu viongozi wa wilaya iwapo wangejaribu kutaka kuniadhibu kwa kumwita Chiligati fisadi. Ni ukweli usiopingika kuwa kati ya watu wanaovuruga CCM Chiligati ni mmojawapo na hana sifa ya kuwa kiongozi ndani ya CC na nasema kuwa niko tayari kuwajibika kwa kusema ukweli dhidi ya Chiligati," alisema diwani huyo.

  Hata hivyo habari zaidi zinasema kuwa diwani huyo anatarajiwa kuitwa wakati wowote kuanzia sasa kujibu tuhuma alizozielekeza kwa Chiligati.

  Wakati wa mkutano wa hadhara, diwani huyo wa CCM alipata nafasi ya kuuliza swali na kuanza kumrushia madongo Chiligati kwamba ni fisadi na ajiuzulu nafasi yake.

  Pia alitaka Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, Andrew Chenge (Bariadi Mashariki) na Rostam Aziz (Igunga) na wengine kufilisiwa mali zao na kunyang'anywa kadi za uanachama.

  Hata hivyo alishindwa kuendelea na hoja yake baada ya baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM kuingilia kati na kusitisha swali lake kwa Chiligati.
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Bora huyo diwani kawa mkweli...
   
 3. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata mimi ninaungana na huyo diwani wa ccm, Chiligati alitufanyia mbaya Manyoni mwaka 2005 kabla ya uchaguzi, alihaidi kuleta msaada wa gari la wagonjwa (Ambulance) lakini ikawa kinyume tukaletewa Mark II used, hilo gari la wagonjwa likayeyukia mjini Dar.
   
 4. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo viongozi wa CCM hawapendi kuambiwa ukweli!!
  Ni lazima ama watamnyang'anya udiwani au kumfukuza kabisa chama!
   
 5. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  huyo diwani ajiangalie,hawa magamba wenzake wanaweza kumchakachua!!
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaa chama kimeshika hatam yatafumuka mengi sana!
   
 7. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Anatimiza na kusimamia ule usemi wa kimombo unaosema THE TRUTH SHALL SET YOU FREE
   
 8. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama ndio hivi basi hapa JF tuna danganyana sana! Siku hiyo ya Tukio la kuanguka Jukwaa mimi mwenyewe Binafsi likuwepo mkutanoni hapo nikiwa na Wandishi wenzangu,kijiji hicho kiko karibu na chuo cha Ihemi ambako Nape na Chiligati walienda kuangalia chuo hicho wakaona waongee na wanakijiji ambapo baada ya Chiligati Kuhutubia alimwita Mwenyekiti Wilaya awasalimie wananchi na badae akamwita Diwani nae asalimie wananchi lakini diwani huyo alikua amelewa chakali na hakuweza kuongea hakuonekana baada ya kuitwa badae akaonekana akiwa chakali! Baada ya kuondoka Nape na Chiligati aliendelea Mbunge wa Jimbo la Kalenga Dr Mgimwa kuhutubia! Jamani hapa JF kumbe tunapeana habari sio za Ukweli nilikuwepo sio kweli na diwani hakusema!
   
 9. m

  mwahajoseph Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yan kuna watu humu JF sijui wanatumwa yan kazi yao ni kutunga story na kubandikaaa hewani kumbe ni uwongoo hii mara ya tatu sasa kwa uzoefu wangu wt wana post vitu vya kizushii tuwe waungwana jaman chuki zitatupeleka pabayaa.
   
 10. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapana Jamani tuwe waaadilifu na Tumuogope MUNGU hata kama ndio siasa jamani mimi nilikuwepo nilichoongea hapo awali huyu diwani hakusema chochote aliitwa akawa amelewa hakuonekana akaja onekana baadae akiwa amelewa balaaa! Kama wamemuita kumjadili kwenye kikao ni labda sababu ya Ulevi!
   
 11. k

  kayumba JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Huyo Diwani unayemsema alikuwa kalewa chakari ndiye anaitwa DENIS LUPALA? isije kuwa tunapewa habari potufu hapa JF!
   
 12. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Kabisa Mheshimiwa Diwani DENIS LUPALA hakusema maneno hayo na alikua amelewa! Naongea kwa Kumuogopa MUNGU hakusema,tusimsingizie huyu Mheshimiwa Diwani. JF kwa namna hii hatuta fika kama ni hivi basi tunaongopeana sana!
   
 13. A

  Abba Member

  #13
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We **** unasemanini? Kwenye post yako ya Dr. Slaa na wizi TEC, mimba ya sista na mke wa mtu. Mbona hujatoa evidence? Mwiba kwa nguruwe kwa binadamu mchungu!

  Pumba.f.u
   
 14. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  CCM Bwana, huyu diwani nadhani alikjuwa anajaribu kuiokoa CCM lakini hawaelewi kuwa wapo gizani!

  Inakuwa CC iliyopita huyu mmoja awe msafi wengine wote wachafu, inakuwa vipi Makamba awe mchafu mwane awe msafi! CCM imeoza inanuka.
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,060
  Trophy Points: 280
  Eti alikuwa amelewa eti habari za uongo wewe unasema hakusema wakati diwani mwenyewe anakiri alisema ajabu kweli, jaribuni kuja na mbinu nyingine za ku distort habari mbinu hiyo haisaidii

  Diwani matatani kwa kumwita Chiligati fisadi
   
Loading...