Herbalist Dr MziziMkavu Platinum Member Joined Feb 3, 2009 Posts 43,111 Reaction score 34,940 Jan 24, 2014 #1 WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe amesema atashughulikia tatizo la polisi kulalamikiwa kula rushwa kwa kuwaandalia mazingira mazuri, ambayo hata akiulizwa kwa nini anakula rushwa hatakuwa na jibu.Chikawe alisema hayo jana,wakati akiripoti katika ofisi mpya kama Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kuteuliwa hivi karibuni, akitoka Wizara ya Katiba na Sheria.Akiwa wizarani hapo alipokewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo , Mbarak Abdulwakil na Naibu Waziri Pereira Ame Silima na wafanyakazi wengine wizarani hapo. Alisema haipaswi kuwa na polisi asiyelipwa mshahara vizuri .Kabla hujaanza kulaumu polisi au mtu yeyote kwa nini anapokea rushwa, ni vema kumtengenezea hali ambayo hata akiulizwa kwa nini anafanya hivyo atakosa jibu.Lakini siyo kama natetea vitendo hivyo, lakini ni vema kujiuliza kwa nini anafanya hivyo alisema. Chikawe aliahidi kupambana na rushwa kadri awezavyo. Alisema kutokana na wizara hiyo kuwa kubwa, siyo rahisi kufahamu kila linaloendelea.Alisema atatoa namba maalumu ya Waziri, kuwasiliana moja kwa moja na wananchi na wafanyakazi walio chini ya wizara yake. Alisema anafahamu wizara ina changamoto nyingi.Alisisitiza atafanya kazi kwa kushirikiana na watumishi wote. Pia alisema atajifunza kutoka kwa Katibu Mkuu na Naibu Waziri, ambao ni wazoefu katika wizara hiyo.http://www.touch.habarileo.co.tz/in...20983-chikawe-kuanza-na-kero-ya-rushwa-polisi Attachments chikawe.jpg 8.3 KB · Views: 159
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe amesema atashughulikia tatizo la polisi kulalamikiwa kula rushwa kwa kuwaandalia mazingira mazuri, ambayo hata akiulizwa kwa nini anakula rushwa hatakuwa na jibu.Chikawe alisema hayo jana,wakati akiripoti katika ofisi mpya kama Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kuteuliwa hivi karibuni, akitoka Wizara ya Katiba na Sheria.Akiwa wizarani hapo alipokewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo , Mbarak Abdulwakil na Naibu Waziri Pereira Ame Silima na wafanyakazi wengine wizarani hapo. Alisema haipaswi kuwa na polisi asiyelipwa mshahara vizuri .Kabla hujaanza kulaumu polisi au mtu yeyote kwa nini anapokea rushwa, ni vema kumtengenezea hali ambayo hata akiulizwa kwa nini anafanya hivyo atakosa jibu.Lakini siyo kama natetea vitendo hivyo, lakini ni vema kujiuliza kwa nini anafanya hivyo alisema. Chikawe aliahidi kupambana na rushwa kadri awezavyo. Alisema kutokana na wizara hiyo kuwa kubwa, siyo rahisi kufahamu kila linaloendelea.Alisema atatoa namba maalumu ya Waziri, kuwasiliana moja kwa moja na wananchi na wafanyakazi walio chini ya wizara yake. Alisema anafahamu wizara ina changamoto nyingi.Alisisitiza atafanya kazi kwa kushirikiana na watumishi wote. Pia alisema atajifunza kutoka kwa Katibu Mkuu na Naibu Waziri, ambao ni wazoefu katika wizara hiyo.http://www.touch.habarileo.co.tz/in...20983-chikawe-kuanza-na-kero-ya-rushwa-polisi