Chief mangungo wa leo

A-town

JF-Expert Member
Oct 25, 2011
494
169
Jamani hivi kunatofauti gani kati ya chief mangungo na viongozi wetu wa leo ambao wanapelekwa hotel na kusaini mikataba mufilis kwa taifa
 
Jamani hivi kunatofauti gani kati ya chief mangungo na viongozi wetu wa leo ambao wanapelekwa hotel na kusaini mikataba mufilis kwa taifa

Kuna tofauti kubwa sana. Chifu Mangungo aliambiwa wanasaini mkataba wa urafiki, kumbe uongo kwani mkataba ulikuwa katika Kijerumani na yeye alikuwa hajui kusoma. Mkapa na first class ya Fasihi ya Kiingereza na Kikwete na shahada yake uchumi wanajua kusoma na Kiingereza na walijifanya kusomea namna ya kufahamu njama za wanyonyaji na mabeberu badala yake wamesaini mikataba ya shanga inayoruhusu kuporwa kwa rasilimali za nchi yetu. Kikwete na mashambenga wake wanasema eti "liwa uliwe." Hata aibu na kujisitahi siku hizi hakupo.
Kwa ufupi mangungo alidanganywa na alikuwa hajui nini anafanya. Mkapa na Kikwete wao wanapigia chapuo sisi "kuliwa." Aibu mbona aibu!
 
Mangungo alisainishwa kitu ambacho aliambiwa uongo, hakujua kwamba anadanganywa, lakini hawa wa sasa wanasaini kitu wanachokijua kwa kupewa rushwa za suti.
 
Wapendwa wanajamii,

Kama ambavyo tunamsoma chifu Mangumgo kwenye historia ya Tanganyika na yale aliyoyafanya,

"NAPENDEKEZA TUWE NA ORODHA YA MAJINA YA WAHUJUMU UCHUMI WANAOUZA NCHI YETU LEO KWENYE HISTORIA YA TANZANIA".

Yaorodheshwe majina yao, yaainishwe madhila ya kila mmoja wao na vizazi vyao, watoto wetu wafundishwe kwenye historia. Aibu hiyo itawafanya viongozi wa kitaifa kufanya kazi kwa manufaa ya nchi. Historia hiyo isifungwe na yeyote atakayejiingiza sasa na baadaye kwenye MATENDO HAYO AINGIZWE kwenye orodha.

Tunayo mengi ya kuandika na mengine yameandikwa humu kuhusu individuals wanaojihusisha na ufisadi unaodidimiza taifa. Tusicheke na nyani, tutavuna mabua.

Nawasilisha
 
Heri ya Mangungo wa msovero asiyejua kusoma kuliko hawa wenyenye kupigania uriba tumbo!
 
Wapendwa wanajamii,

Kama ambavyo tunamsoma chifu Mangumgo kwenye historia ya Tanganyika na yale aliyoyafanya,

"NAPENDEKEZA TUWE NA ORODHA YA MAJINA YA WAHUJUMU UCHUMI WANAOUZA NCHI YETU LEO KWENYE HISTORIA YA TANZANIA".

Yaorodheshwe majina yao, yaainishwe madhila ya kila mmoja wao na vizazi vyao, watoto wetu wafundishwe kwenye historia. Aibu hiyo itawafanya viongozi wa kitaifa kufanya kazi kwa manufaa ya nchi. Historia hiyo isifungwe na yeyote atakayejiingiza sasa na baadaye kwenye MATENDO HAYO AINGIZWE kwenye orodha.

Tunayo mengi ya kuandika na mengine yameandikwa humu kuhusu individuals wanaojihusisha na ufisadi unaodidimiza taifa. Tusicheke na nyani, tutavuna mabua.

Nawasilisha
 
lakini kwanini huyo Mangungo nae asaini bila kujua kusoma? Inaonyesha kwamba pia alikuwana tama, huwezi kufanya kitu usichojua madhara yake. Ndio maana Nyerere alikataa kuanza kuchimba madini kabla hatujawa na ujuzi na uwezo huo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom