Nakumbuka drs la tano, nlikuwa stuborn saana pale Nyakabungo mwanza lazima nipite kwenye mazenga ya mikate kwa Ally said. Sasa nikiwa na mazenga mara mwl mkuu huyu hapa Aron akiwa na kigari chake kilichochoka. Jamaa alikuwa anatisha kwa bakora dunia nzima.
Nilishangaa siku hiyo kwani alikuwa very friendly akaniuliza nina shida gani nkamwambia nimefiwa na ninarudi nyumbani, nkasikia ohooo pole sana mtoto!! Twende dukani nikakununulie jojo twende shule nikaandike msiba kwenye vitabu. Nikafanya kosa kubwa saana kurudi shule na mwl mkuu.
Nlichapwa kichwa kikiwa ndani ya desk kama nimechoma shule makusudi viiile. Aiseeee!