Uchaguzi 2020 Cheyo atoa wito kwa Wananchi kumpa kura Dkt. Magufuli

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP), John Cheyo amewaomba wananchi wa Jimbo la Itilima, kumpigia kura mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli kwa kuwa anatekeleza anayoahidi na anajali shida za wanyonge.

Aliyasema hayo katika Kijiji cha Inalo Kata ya Lugulu wilayani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Itilima kupitia UDP, Simon Ngagani.

Cheyo alisema UDP wamekubaliana kumuunga mkono Magufuli kutokana na jitihada zake kusikiliza wanayoyataka wananchi, wakiwamo wanasiasa wa upinzani. Alisema baadhi ya mambo hayo yamo ambayo wanasiasa wa upinzani akiwamo yeye wameyapigia kelele miaka ya nyuma.

"Tuna sababu kubwa ya kumuunga mkono Dk Magufuli kwani kwa kipindi cha miaka yake mitano ya uongozi, tayari ameshatekeleza kwa vitendo sera ya elimu bure, huduma za afya na uboreshaji wa miundombinu rafiki na wezeshi ya biashara,” alisema.

Hata hivyo, Cheyo alisema haridhishwi na mfumo uliopo ununuzi na ulipaji wa fedha za wakulima wa pamba, kwa madai kuwa unachelewesha kupata haki yao.

Mgombea Ubunge Jimbo la Itilima, Ngagani aliwaomba wananchi wamchague ili ashirikiane nao kuliletea maendeleo jimbo hilo.

Ngagani alisema ameacha kazi baada ya kuona changamoto kwenye jimbo hilo, hivyo endapo atachaguliwa atahakikisha anasimamia uanzishwaji wa viwanda na miradi ya maendeleo ili kumaliza tatizo la ajira.
 
Hao wananchi wanaoambiwa maneno hayo,inabidi mkiwaona waambieni ,sababu ya kuambiwa maneno hayo ni huyo anafaidika yeye pekee tu.
 
Rais wetu ni huyu
IMG-20200911-WA0014.jpg
 
Cheo amelianzisha ,CCM wataona ni sawa hivyo kupigiwa debe na wagombea wa vyama vingine.Natarajia na Lipumba atafanya hivyo hivyo na Mbatia.

Sasa na sisi Wapinzania wa KweliTutampigia debe Lisu na Kumuunga mkono ,lakini tuwaomba tume wasije kutushobokea .
Kama hili nikosa basi na lile nikosa waanze na haokwanza.

Membe, Kumuunga mkono lisu Kuanzia Muda wowote.
 
Huyu naye ukabila unamsbua. Alimpinga sana JK, leo haoni atrocities zozote katika utawala huu wa msukuma mwenzake
 
Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP), John Cheyo amewaomba wananchi wa Jimbo la Itilima, kumpigia kura mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli kwa kuwa anatekeleza anayoahidi na anajali shida za wanyonge...
Huyu si mshauri wa siasa wa magufuli...akafie mbali huko bariadi..kwanza alikuwa mwizi na mfilisi wa.mwatex akakimbia Tanzania wakati wa nyerere..mwizi mkubwa huyu ..kazi watoto kumnyonya.
 
Back
Top Bottom