Cheti cha ndoa cha kutoka BAKWATA kinatambulika Serikalini?

Abuwhythum

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
837
495
Mimi ni mwanandoa, tulifunga ndoa ya kiislamu na kupata cheti cha ndoa kutoka BAKWATA. Ninahitaji kumhamisha mke wangu ambaye ni mfanyakazi serikalini ili tuishi pamoja. Je cheti hiki tulichonacho kitafaa kutambulika serikalini? Au ni lazima tuwe na cheti kutoka RITA?

Naomba msaada wenu juu ya suala hili.
 
Mkuu unapofunga ndoa nazani huwa wanatoa vyeti viwili kimoja cha serikali na kingine na BAKWATA au Kanisa, ila nazani ulizia pia mana serikali inatambua ndoa ya kidini na kimila jaribu fuatilia kwa ukaribu zaidi, au irumba tusaidie ufafanuzi zaidi
 
Mimi ni mwanandoa, tulifunga ndoa ya kiislamu na kupata cheti cha ndoa kutoka BAKWATA. Ninahitaji kumhamisha mke wangu ambaye ni mfanyakazi serikalini ili tuishi pamoja. Je cheti hiki tulichonacho kitafaa kutambulika serikalini? Au ni lazima tuwe na cheti kutoka RITA?

Naomba msaada wenu juu ya suala hili.

Kinatambulika brother!!
Mimi ni mwajiriwa serikalini, nlifunga ndoa ya kiislamu na nikapewa cheti cha BAKWATA kama wewe ulivyopewa.

Baada ya ndoa, niliwasilisha cheti nilichopewa na BAKWATA kwa mwajiri wangu kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi.

Kilipokelewa na mwajiri wangu akanipa barua ya kukiri kukipokea cheti changu.

Lakini pia, nimekuwa nikilipwa stahili zangu zote zinazohusishwa mwenza wangu. Mfano, fedha ya likizo (mke wangu pia atapata) na hata fedha za kujikimu pale ninapohamishwa amekuwa akilipwa pia.

Nipo katika ndoa, mwaka wa nane sasa.

Cheti cha BAKWATA na vinavyotolewa na taasisi nyingine za kidini vina hadhi sawa na cheti cha RITA
 
Wafungisha ndoa wote ni mawakala wa RITA ukisha funga ndoa wakala anatakiwa kuwa na vyeti vyote viwili cha kwake na cha RITA
Ikitokea ikawa hana basi unakwenda na cheti cha wakala kusajili RITa
 
Kinatambulika brother!!
Mimi ni mwajiriwa serikalini, nlifunga ndoa ya kiislamu na nikapewa cheti cha BAKWATA kama wewe ulivyopewa.

Baada ya ndoa, niliwasilisha cheti nilichopewa na BAKWATA kwa mwajiri wangu kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi.

Kilipokelewa na mwajiri wangu akanipa barua ya kukiri kukipokea cheti changu.

Lakini pia, nimekuwa nikilipwa stahili zangu zote zinazohusishwa mwenza wangu. Mfano, fedha ya likizo (mke wangu pia atapata) na hata fedha za kujikimu pale ninapohamishwa amekuwa akilipwa pia.

Nipo katika ndoa, mwaka wa nane sasa.

Cheti cha BAKWATA na vinavyotolewa na taasisi nyingine za kidini vina hadhi sawa na cheti cha RITA

Mkuu shekh alipaswa kukupa vyeti vyote viwili
 
Cheti knachotolewa msikiti,kanisani na kwa dc vyote vinatoka serikali..so kinatumika bro
 
Kinatambulika brother!!
Mimi ni mwajiriwa serikalini, nlifunga ndoa ya kiislamu na nikapewa cheti cha BAKWATA kama wewe ulivyopewa.

Baada ya ndoa, niliwasilisha cheti nilichopewa na BAKWATA kwa mwajiri wangu kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi.

Kilipokelewa na mwajiri wangu akanipa barua ya kukiri kukipokea cheti changu.

Lakini pia, nimekuwa nikilipwa stahili zangu zote zinazohusishwa mwenza wangu. Mfano, fedha ya likizo (mke wangu pia atapata) na hata fedha za kujikimu pale ninapohamishwa amekuwa akilipwa pia.

Nipo katika ndoa, mwaka wa nane sasa.

Cheti cha BAKWATA na vinavyotolewa na taasisi nyingine za kidini vina hadhi sawa na cheti cha RITA

sio kweli chet kinachohtajka kwa mtumishi ni chet cha ndoa cha serikali hats hivyo unatakiwa wakat unafunga ndoa upewe chet cha dini na cha serikal labda Huyo mwajiri wako sheria zimempitia pemben na kama huamin hili ingia kwny Google utafute RITA Tanzania uwaulize
 
Mimi ni mwanandoa, tulifunga ndoa ya kiislamu na kupata cheti cha ndoa kutoka BAKWATA. Ninahitaji kumhamisha mke wangu ambaye ni mfanyakazi serikalini ili tuishi pamoja. Je cheti hiki tulichonacho kitafaa kutambulika serikalini? Au ni lazima tuwe na cheti kutoka RITA?

Naomba msaada wenu juu ya suala hili.
bofya hapa kupata kitabu kinaongelea yote hayo SHERIA TANZANIA
 
Back
Top Bottom