Cheti cha kufundisha kiswahili kwa wageni chakosesha ajira kwa watanzania wengi nje ya nchi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Nchi nyingi ukienda ukiomba kuwa mwalimu wa kiswahili utaulizwa kama una cheti cha kufundisha kiswahili kwa wageni.

Wakenya wajanja vyuo vyao vikuu hutoa hicho cheti unasoma miezi mitatu kama sikosei.Wakenya wengi wanaosafiri nje husomea hicho cheti na kupata kazi sehemu nyingi tu za kufundisha kiswahili.

Tanzania kuna chuo kinachotoa hicho cheti? Kama kipo kijitangaze sana na kihakikishe ikiwezekana kila mwanafunzi anayemaliza chuo kikuu apate nafasi ya kusoma na kupata hicho cheti.Chaweza kumsaidia nchi zingine kama kinavyowasaidia wakenya.Badala ya kuwa mbeba box akawa mwalimu wa Lugha ya kiswahili
 
Wee acha tuu, yaani hata wakalimani wa kiswahili ni Wakenya na kiswahili chao kibaya na huku nilipo nimekuta wabongo wengi kama mvua lkn hamna hata mmoja, ukikutana na mtu ukasema unaongea kiswahili swali la kwanza ni "are you from KENYA" !!!!!!?????
 
Hicho cheti kinatolewa udsm, unasoma kozi inaitwa swahili applied linguistic , unasoma kwa miezi 3 mwishoni unapewa cheti

Wajitangaze sana kwenye TV,RADIO NK hicho cheti kina soko kubwa nje.Wakenya mtu hata akimaliza form four hukimbilia kusomea hicho cheti.Hicho cheti ni hot cake.Mtu ukisafiri nje ukiwa nacho unaaminika kuwa una uwezo wa kufundisha kiswahili na kuwa mkalimani nk

Hiyo programme wakiitangaza vizuri watapata wanafunzi wengi mno.Walimu wote wawe wa sekondari ,msingi na wanavyuo wote ni vizuri wawe na hicho cheti.

Na hata vijana waliomaliza kidato cha nne au sita wakasomee hicho cheti kitawasaidia wakikanyaga nchi yoyote kuweza kuomba nafasi za kufundisha kiswahili.

Hicho cheti ni Mgodi mwingine kama wa Tanzanite
 
hilo mbona ni tatizo dogo sana wasiliana na baraza la kiswahili Tanzania watakupa jibu

kuwasiliana,kuwasiliana ukiritimba kwenye kila kitu.Kama una taarifa toa hapa.Au hilo baraza lilete hizo taarifa hapa na lisambaze taarifa kwa kwa wingi ziwafikie watu wengi.Jambo muhimu kama hili wanalifanya kama uchawi.

Tunazidiwa na wakenya wasiojua kiswahili vizuri kisa ukiritimba wa kijinga wa kuficha ficha taarifa wa Baraza la kiswahili!!

sema baraza linasaidiaje katika hili ili watu wetu wapate nao ajira nje za kufundisha kiswahili kwa wageni
 
Back
Top Bottom