Cheo cha Katibu Mkuu Kiongozi kifutwe

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
Cheo cha:
KATIBU MKUU KIONGOZI KIFUTWE.

Sioni tija uwepo wa cheo hiki, ikiwa Msemaji Mkuu wa SERIKALI bungeni ni Waziri Mkuu ambaye pia kimamlaka ana sauti kubwa nje ya bunge kuliko Katibu Mkuu Kiongozi ambaya ana deal na watumishi wa Umma kitu ambacho kinafanywa na Nafasi ya Waziri Mkuu.

Nchi yetu ina Rais, hivyo Mtendaji Mkuu wa SERIKALI ni Waziri Mkuu. Nchi za kifalme zina Waziri Mkuu, hivyo kwao anakuwepo Katibu Mkuu Kiongozi kama msimamizi wa SERIKALI. Sasa kwetu sisi tuna copy na Ku paste kila cheo bila kujua mfumo tunao copy.

Napendekeza cheo hicho ni bora kifutwe kupunguza na matumizi yasiyo ya lazima ndani ya SERIKALI.

Jioni njema:
Deogratius N Kisandu.
 
Serikali sio watumishi was uma tu katibu mkuu kiongozi anasimamia watumishi wa uma na maswala ya utumishi.waziri mkuu serikali na mambo yahusuyo serikali kwa ujumla wake vipi ulinganishe pm na Km kiongozi?
 
Hivi unafahamu kazi katibu mkuu kiogozi, au na wewe umeamua kuanzisha thread tu?
 
Serikali sio watumishi was uma tu katibu mkuu kiongozi anasimamia watumishi wa uma na maswala ya utumishi.waziri mkuu serikali na mambo yahusuyo serikali kwa ujumla wake vipi ulinganishe pm na Km kiongozi?
HILI NDILO JIBU. Bila Katibu Mkuu utendaji wa utumishi wa umma utakosa kiongozi kimsingi huyu ni kama CEO wa watumishi wote wa Umma. Hakuna taasisi isiyokuwa na Kiongozi wa juu!
 
Ma DC RC ndio hawana kazi na hawastahhili kuwepo! Mrundikano tu watu wamejazana wanafanya kazi sio zao wao hawana kazi!!!
 
Kwa leo huyu jamaa ameongea kitu ambacho hata mimi kinanikwaza, tuna Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi, hawa wote ni gharama sana kuwa nao.
 
Huyu jamaaa hajielewi kwa kifupi alitakiwa afatilie kwanza kabla ya kuongea humu kwahy anaona katibu mkuu ni mkbw kwa PM
 
Back
Top Bottom