Hakunaga kitu kinaniuma kama kumuachia konda chenji yangu hata ikiwa sh 50 na sijui kwanini yaani hata nikiwa nimetoka kupiga dili la milioni kumuachia konda da inaniuma sana yaani no bora niiche kwa mangi tu dukani !! Hivi hii situation ni kwangu tu au hata na wewe mwana jf mwenzangu ..kwanini tunadai sana chenji zetu ni bora ukaitupe kuliko kumuachia konda !!! Tatizo ni nini haswa !!
Karibuni
dili la milioni unapanda daladala? au za zimbabwe?
mi nachukia sana. wao ukipungukiwa mia wanakataa kabisa
Mi nagawana nao pasu, nikipanda asiniulize nauli nakausha.
Na hii ilitokea baada ya kusahau chenji ya Shs 10,000 kwenye dala dala ya Mwananyamala - Kivukoni mwaka 2007 mpaka leo inaniuma na sina uhakika kama nilisha irudisha. Lakini najua itarudi tu.
Tafuta noti feki mpwa zinarudi
Ukizungusha basi Tatu kwa noti za 10"000 unapata halali 9000 *3 -sawa na 27"000
Panda sheki shuka mapambano....akirudisha weka mfuko wa kushoto
Panda lingine elekea mtogole ukipewa chenji weka mfuko wa nyuma
Hii ya Tatu panda kwa mtogole shuka ubungo atakaporudisha chenji hapohapo shuka kinachofwata
Piga 27"000 Mara 30 ujanunua ile bar ya ngirawanecha kama akili nyingi za kichaga
Kwa hiyo wewe ukiwa na shilingi za Kitanzania kuanzia milioni moja daladala hupandi? Kweli ulimbukeni ni janga nalo!!!!
Milioni unaona pesa we kweli cha ukucha !! Ushazoe dili zako za buku jero unaenda kwa pusha kupata mambo yako !! Ukipewa million utaomba escort ya jwtz wewe
dili la milioni unapanda daladala? au za zimbabwe?
Heee kwa hiyo wewe ukipiga dili la milioni unanunua gari ama...? Milion ni kitu gani kwanza kwa hapa mjini
Duh!,kwa hiyo mkuu kila unapofanikiwa kukausha huwa unaweka rekodi!,nimeipenda,ila ukweli huwa inauma!Mi nagawana nao pasu, nikipanda asiniulize nauli nakausha.
Na hii ilitokea baada ya kusahau chenji ya Shs 10,000 kwenye dala dala ya Mwananyamala - Kivukoni mwaka 2007 mpaka leo inaniuma na sina uhakika kama nilisha irudisha. Lakini najua itarudi tu.
Naachaga sana Mia mia mbili kama hana chenji namwachia...
Wala roho haiumi