Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,814
- 34,196
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) jana, ilishindwa kutoa majibu ya
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu
Dodoma. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) jana, ilishindwa kutoa majibu ya moja kwa moja kuhusu ahadi ya Serikali ya kupeleka madawati ya chenji ya rada kwenye halmashauri mbalimbali nchini.
Swali hilo liliulizwa na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itakamilisha ahadi yake kwa kupeleka madawati 708 kwa kila wilaya yaliyotakiwa kununuliwa kutokana na fedha hizo.
Lissu alisema katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambako pia kulikuwa na ahadi ya aina hiyo, hakuna hata dawati moja ambalo lilinunuliwa na hajui mpango huo uliishiwa wapi.
Awali, Serikali iliahidi kupeleka madawati 708 kwa baadhi ya halmashauri za wilaya yakiwa katika muundo wa plastiki.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alisema mpango huo bado upo na kwamba, kuna shule ambazo zilipelekewa madawati kama ilivyotakiwa.
Hata hivyo, alisema atapitia kuangalia ahadi katika baadhi ya maeneo, ikiwamo kupeleka bungeni mkakati maalumu wa Serikali ya Awamu ya Tano utakaohakikisha kuwa tatizo la madawati kwa shule za msingi na sekondari linakwisha.
Sh78.7 bilioni zilizozidi kununulia rada wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu maarufu kama ‘chenji ya rada’ zilirudishwa kwa Serikali ya Tanzania na kampuni ya kutengeneza vifaa vya kivita ya BAE Systems ya Uingereza.
Katika hatua nyingine, Serikali imetoa nafasi kwa baadhi ya wazazi na wadau wengine kuchangia michango ya upatikanaji wa madawati kwa kadri watakavyoona inafaa ilimradi wasisumbue au kufanya michango hiyo iwe kizuizi cha kupeleka watoto shule.
Wito huo ulitolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya wakati akijibu swali la Mbunge wa Ndanda (Chadema), Cesil Mwambe.
Mbunge huyo alitaka kujua Serikali imejipanga vipi kuhakikisha wanafunzi hawarudishwi shule kwa sababu ya michango ya mlinzi, madawati na chaki.
Naibu waziri alisema hakuna mkuu wa shule ambaye atamrudisha mwanafunzi nyumbani kwa kutolipa michango ya mlinzi, madawati na chaki kwa sababu majukumu hayo ni ya Serikali.
Chenji ya rada yaibuka bungeni