Asante kwa kunikumbusha juu ya chanzo cha swali. Samahani kwa kukukosea katika hii.
a)Hapana Marekani imekimbia utaratibu wa ICC. Bado wanajisikia ni wakuu hawataki kukubali wengine kuwahukumu.
b) si sahihi ya kwamba ICC ilikuwepo kabla ya 1998/ 2002. Labda unaichanganya na Mahakama Kuu ya Kimataifa (International Court of Justice kifupi ICJ)? Chanzo chako si wazi hapa.
a) Ukiona kanuni za ICC hakuna msingi wa kupeleka kesi hii huko. Marekani ipende isipende!
Chungulia mwenyewe kanuni uniambie ICC ingeangalia mambo ya Ali kwa msingi gani??
B) Tena sioni ya kwamba Ali alihukumiwa haraka sana. Inaonekana kuna watu wengi huko Iraq waliotaka kumalizana naye mbele ya mahakama - maana hawakumnyonga baada ya hukumu ya kwanza ilitotolewa mwaka 2007 (leo 2010!).
c) Wakurdi walitaka ufafanuzi kuhusu matumizi ya gesi ya sumu (wakati ule Marekani hakika ilitafuta tamko hili pia kama uthebitisho wa vita yake)
d) Lakini Washia walipotafuta ufafanuzi rasmi mbele ya mahakama haikuwa habari rahisi kwa Marekani maana Washia wanashikamana na Iran adui wa Marekani.
Pia ni wazi hata Marekani iliwajibika kwa namna fulani katika vifo hivi maana wakati ule 1991 Marekani iliwapa moyo Washia kusimama dhidi ya Saddam bila kuwasaidia wakachinwa.
Mkuu
Kipala,
swali: Si msingi wa kupeleka hizi kesi ICC ingekua crimes against humanity?
Kwani what is the difference kati ya huyu bwana na kina Milesovic?
Mie nakubaliana nawe 100% kua marekani wana double standards when
it comes to ICC. Maana jeshi lao likiua watu kimakosa they are not
subjected to prosecution on foreign soil lakini watalazimisha nchi zengine
kuenda huko.Hapo tuko pamoja.
Kuhusu chanzo cha ICC mimi nimechukua mtazamo kama mwalimu wa
Historia na arguments zangu hata nilipokua college nilikua nabisha hivyo.
Technicalities are based on the names. Zile Nuremberg trials za baada
ya WW II were a mirror image of the ICC...ICJ/ICC kwangu ni kitu kimoja.
Nakumbuka nikimwambia lecturer wangu kua League of Nations na United
Nations is just the same thing..difference ni jina na mahala headquarters
ilipo. Hata hivyo I understand where you are coming from.
Kuhusu ishu ya 'uharaka', Im reflecting on Saadam Hussein. Hamna cha kukata
rufaa wala nini. When it comes to International Courts, kesi zinaweza
ku-drag for an untold time lakini zikiwa humuhumu uswahilini
mwetu tutazikimbiza na hata tukikiuka sheria, they are not really
answerable to anybody. Nd'o mtazamo wangu hapo.
Shukran kwa kuelimishana hapo mkuu.
Tuzidi.