Chelsea wakomba tuzo tatu za ligi kuu novemba...haijawahi kutokea!

118cc03a0a58a96d2078c696581dcc0a.jpg


Kutoka kulia Costa, Conte na Pedro wakiwa na
tuzo zao Uwanja wa mazoezi wa Cobham leo
baada ya kukabidhiwa

KITENDO cha Chelsea kupaa kileleni mwa Ligi
Kuu ya England kimeleta faida kubwa, kwa
klabu hiyo kushinda tuzo tatu za mwezi Novemba.

Diego Costa amekuwa Mchezaji Bora wa Mwezi
Novemba, wakati Antonio Conte amekuwa
Kocha Bora na Pedro ameshinda tuzo ya Bao
Bora la Mwezi alilofunga katika ushindi wa 2-1
dhidi ya Tottenham.

Tuzo hizo zinazotokana na kura za mashabiki
na wataalamu, zinakuja mwezi mmoja baada ya
Conte na mchezaji wake nyota, Eden Hazard
kushinda tuzo za Mchezaji Bora na Kocha Bora
kwa mwezi Oktoba.

Hii inakuwa mara ya kwanza tuzo zote tatu
zinakwenda kwa klabu moja na inafuatia
Chelsea kushinda mechi zote tatu za Ligi Kuu
mwezi Novemba - wakiichapa Everton 5-0 kabla
ya kuzifunga na Middlesbrough na mahasimu
wao wa London, Tottenham.
Waliendeleza wimbi lao la ushindi la Novemba
na kwa kushinda mchezo wao wa kwanza wa
Desemba wakitoka nyuma na kuifunga
Manchester City 3-1 Uwanja wa Etihad.
Costa, ambaye alifunga mabao mawili katika
mechi tatu za Chelsea Novemba, alisema baada
ya kupokea tuzo yake: "Mambo yanakwenda
vizuri kwa sasa.

Timu inafanya vizuri na hii
inaonyesha kwamba mambo yananinyookea,".
 
'blue is the colour, football is a game!'.........ma-blues mpoooo? Mwaka huu ni wetu!!
 
Kwa sasa Chelsea wako njema sana. Huenda ndio Best Club kwa sasa katika ligi zote katika nchi za Ulaya.
 
Back
Top Bottom