Cheka sana, kula raha sana, Ruka sana, Tamba sana, Jirushe sana, Fanya starehe sana ila Omba ukiugua usije kupatiwa Matibabu kwenye Hospitali zetu!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!.

Cheka sana tu, ruka huku na huko sana tu, Puyanga sana tu,Fanya ngono sana,Kunywa pombe sana tu,Fanya uasherati sana tu,Jifariji sana tu kwa mambo ya kijinga,zembea sana tu,dharau sana tu!.

Ila omba kwa dini yako sana tu usije ukaugua ukalazwa au kupatiwa matibabu kwenye hospitali za serikali,Utajuta!.

KUMBUKA- Ukiwa kwenye starehe jitahidi kusevu na hela kwa ajili ya matatizo kwasababu matatizo yapo tu hivyo yanapaswa yawe na bajeti yake kama ambavyo starehe umeitengea bajeti.

Kwa wakazi wa Dar usiombe upelekwe MWANANYAMALA,AMANA,TEMEKE.

Narudia tena UTAJUTA.

Kwenye video hapa chini ni muhudumu ambaye anaosha vifaa vya upasuaji kwa maji baridi na sabuni bila hofu yeyote,vifaa hivyo ndivyo vitakavyotumika siku umelazwa kufanyiwa upasuaji eidha iwe wewe au mkeo.

Hapa ni AMANA HOSPITILI ILIYOKO DAR ES SALAAM sijajua huko mikoani hali ikoje!







Yangu ni hayo tu.
 
inaonekana kwenu mnakufa na magonjwa ya zinaa na pombe, imekuuma hadi umekuja kutujazia wosia JF, ukidhani wote wanao umwa ni sababu ya starehe mbaya 🤣😅 tafuta pesa uishi maisha mazuri ili usionee wivu watu na starehe zao
 
Back
Top Bottom