Mkuu yaani na mimi nilitaka kuangukia hapo hapo hebu labda niambie ina nini hasa??Sio nzuri au ipoje??maana labda nijue kabla sijanunua
Mimi nimechukua kimoja jana (Newsmy Newpad P9) 8" kwa mshkaji alitaka nimpe 500,000 ila baada ya kukaa nacho usiku mmoja tu nimeamua leo nimrudishie. Yaani kama alivyosema mdau hapo juu hiki ni ki toy tu hamna kitu. Bora kama vipi utafute tu ka mini laptop kazuri utaenjoy kuliko hivi vitakataka.
Baadhi ya matatizo ni haya:
1. Kwa sisi wabongo tuliozoea windows kitakusumbua maana huwezi kuinstall applications ulizozizoea zaidi ya office
2. On screen keyboard ni ngumu sana kutumia maana kitu chenyewe kiko flat na vi key ni vidogoooo..kazi kwelikweli.
3. Yakwangu ina ka external keyboard ila na kenyewe ni kadunchu yaani key ziko kama piriton
4. Uzito wake ni kama gram 500 na zaidi. Unaweza kudhani ni uzito mdogo lakini mfano unasafiri kwenye basi, na unataka kuangalia movie, kushikilia gram 500 mkononi safari nzima si kazi ndogo!
5. Internal memory bado ni ndogo inabidi ununue memory card au external hdd
6.Kwa jinsi kalivyokaa, sioni mahali pa kufungulia incase unataka kuchokonoa. Sidhani kikiharibika kinafaa kutengeneza
7. Upatikanaji wa spea zake mfano chaja, nadhani ni shida
8. Chakwangu haki support modem! na wala hakina port ya internet. only wireless
9. Betri inakaa 6 hours max