Kenya 2022 Chebukati asimulia yaliyomkuta kabla ya kutangaza matokeo urais Kenya

Kenya 2022 General Election

Super Don

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,978
1,780
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati amedai Jumatatu ya Agosti 15, 2022 alihangaishwa akiwa pamoja na makamishna na wafanyakazi wa tume hiyo ya uchaguzi.

Chebukati amewataja makamishna wawili, Bolu Moya na Profesa Abdi Guliye pamoja na afisa mkuu wa IEBC Marjan Hussein kuwa walijeruhiwa na baadhi ya viongozi wa Azimio walipowavamia katika jukwaa la kutangazia matokeo ya urais.

Chebukati ameeleza kuwa baadhi ya maofisa wa IEBC walikamatwa kiholela hata katika ukumbi wa Bomas na wengine kupewa vitisho.

Katika tukio la Jumatatu ambapo maofisa wa IEBC walijeruhiwa, vurugu zilianza baada ya maajenti kinara wa ODM, Raila Odinga kuanza kuzozana baada ya Chebukati kufika katika ukumbi kutangaza matokeo.

Maajenti hao walidai Chebukati alitoweka kwa muda kabla ya kuwapa fomu za matokeo ili wakague na walipomwona katika ukumbi huo wa Bomas walianza kumuandama wakimtaka awaonyeshe fomu hizo.

Vurugu zilizuka seneta mteule wa Narok, Ledama Ole Kina, gavana mteule wa Siaya, James Orengo na maajenti wengine wa Odinga walipomshambulia Chebukati, makamisha na maofisa wa IEBC.

Vurugu hizo zilifanya matangazo ya uchaguzi kucheleweshwa hadi saa kumi na mbili jioni kinyume na alivyotangaza awali na Chebukati.
 
Nawasikitikia wakenya masikini. Ruto amewekwa na matajiri wakikuyu. Wajiandae
 
Chebikate kachakachua Uchaguzi wa KENYA kwanini Atofautiane na Makamishina Wenzake?
 
Back
Top Bottom