Ndomana mpaka sasa msumbiji wanaitaka Ile nyumba aliyofia mondlane ambayo kwa sasa inamilikiwa na tajiri wa kihindi murtazaEduardo Mondlane (mwanzilishi wa chama cha kupigania uhuru Msumbiji cha FRELIMO akiwa na Ernasto Che Guevara katika ofisi za FRELIMO jijini Dar es salaam mwaka 1966. Che Guevara alikuwepo Dar es salaam kwa miezi 5 kati ya mwaka 1965 hadi 1966. Akiwa Dar es salaam Che Guevara alitumia jina la siri ( code name) '' TATU '' ni jumla ya herufi katika jina C, H, E (CHE). Alikuwa mteja wa mara nyingi katika mgahawa wa Zahir ulipo katika mtaa wa msikiti jijini Dar es salaam ( mgahawa huo bado upo) na aliishi katika ubalozi wa Cuba, kutoka Dar es salaam, Che Guevara alielekea Congo. Eduardo Mondlane aliuwawa kwa bomu jijini Dar es salaam ambalo lilitegwa katika kitabu alichotumiwa toka Ujerumani Magharibi na alizikwa makaburi ya kinondoni. Nafasi yake ya uongozi wa FRELIMO ili chukuliwa na Samoa Machel
Ndomana mpaka sasa msumbiji wanaitaka Ile nyumba aliyofia mondlane...
Ndomana mpaka sasa msumbiji wanaitaka Ile nyumba aliyofia mondlane ambayo kwa sasa inamilikiwa na tajiri wa kihindi murtaza
Mleta mada Kuna mzee wangu mmoja anakaa
Mikocheni pale azura anamjua vizuri mondlane
Maana mpaka tukio lile la kulipukiwa na bomu wakati huo walikuwa ma jirani.
Ukitaka stori za mondlane anazo nyingi. Kweli mleta mada hii umenigusaaa jamaa alikuwa shujaa
Mkuu unaweza ukamuuliza story zake ukazimwaga humu? Hiyo nyumba ipo maeneo gani alipofia Eduardo Mondlane?
Mkuu unaweza ukamuuliza story zake ukazimwaga humu? Hiyo nyumba ipo maeneo gani alipofia Eduardo Mondlane?
Ilikuwa wapi hyo nyumba mkuu??
Ipo wapi ? hapa tz
Alishindwana na wakongo kutokana na tabia yao ya kuendekeza anasa hata kwenye issue serious,che aliwahi kuelezea kuwa wakati alipokuwa msituni kongo akiwafunda askari wa ki mapinduzi,ilipofika jioni wale askari walimtaka waagane ili waende mjini kuserebuka kusaka mademu!! Che akaona hawa viumbe bado hawajahitaji mapinduzi ki ukweli,hivyo akaachana nao na ndipo alipopitia TZ on the way kurudi zake kwao,pia alipitia zanzibar, NB hata wakati alipokuwa safarini kuelekea huko congo alipitia hapa pia.Alitoka Congo ndo akaja tz..
Alishindwana na wakongo kutokana na tabia yao ya kuendekeza anasa hata kwenye issue serious,che aliwahi kuelezea kuwa wakati alipokuwa msituni kongo akiwafunda askari wa ki mapinduzi,ilipofika jioni wale askari walimtaka waagane ili waende mjini kuserebuka kusaka mademu!! Che akaona hawa viumbe bado hawajahitaji mapinduzi ki ukweli,hivyo akaachana nao na ndipo alipopitia TZ on the way kurudi zake kwao,pia alipitia zanzibar, NB hata wakati alipokuwa safarini kuelekea huko congo alipitia hapa pia.
Upo sawa mkuu Lakin kabla ya kwenda pia alipitia Tanzania then ndo akaenda CongoAlitoka Congo ndo akaja tz..