Chawa wa kichwa wananidhalilisha naombeni msaada

petrop1

Member
Apr 27, 2020
50
9
Mimi ni kijana wa miaka 26..Mwaka 2012 nilipatwa na tatizo hili la chawa katika mwili kimaajabu ila kufikia 2014 tatizo lilibadilika chawa wakawa ni wa kichwani (kwenye ngozi ya kichwa)..nimetumia kila dawa kila mbinu ninayoamini ingenisaidia nmegonga mwamba.

Inafikia hatua naogopa hata kujichanganya penye watu maana wadudu hawa huwang'ata pia ninaokutana nao okipelekea watu kuanza kujikuna sehemu mbalimbali mwilini ninapokuwa nipo nao.

Kwa kutambua ukubwa wa jamii forum nmeleta hu uzi nikiamini nitasaidiwa..naahidi ataenisaidia nipone kabisa nipo tayari kumfanyia kazi bure mwaka mzima..asanteni sana
 
Chawa Na Mayai Yake
Chukua unga wa Habbat-Sawdaa uliosagwa vizuri ukande kwenye siki mpaka uwe kama Kremu, halafu ujipake kichwani – baada ya kunyoa nywele au kuisugua kwenye mashina ya nywele, halafu ukae katika mwanga wa jua kitambo cha robo-saa. Na utaosha kichwa ila baada ya masaa matano. Atafanya hivyo kila siku kwa muda wa wiki moja chawa wote watakimbia.
 
Kijana wa mikoani umefeli wapi?
Umenikumbusha kitambo sana😂

😂Anyway..nyoa nywele za sehemu zote. Tena kipara. Chemsha maji ya Moto. Tena sana! Ingiza nguo zako zote,mito,foronya na godoro (kama unavyo). Tafuta dawa ya unga kuua vijidudu (k.v utitiri,kupe,) mwagia chumbani kwako Kila Kona na sehemu.

Mwisho uwe unakoga brother! Na sabuni🤣🤣🤣
 
nilijua nimeyaona yote lakini mpakamuda huu siwajui wala sjawah kuwaona hao wadudu nisaiidie picha yaomkuu


Nawewe acha ushamba, hivi kweli hujaona chawa???!!😒

Screenshot_20210107-211808.png
 
Mimi ni kijana wa miaka 26..Mwaka 2012 nilipatwa na tatizo hili la chawa katika mwili kimaajabu ila kufikia 2014 tatizo lilibadilika chawa wakawa ni wa kichwani(kwenye ngozi ya kichwa)..nimetumia kila dawa kila mbinu ninayoamini ingenisaidia nmegonga mwamba..inafikia hatua naogopa hata kujichanganya penye watu maana wadudu hawa huwang'ata pia ninaokutana nao okipelekea watu kuanza kujikuna sehemu mbalimbali mwilini ninapokuwa nipo nao...kwa kutambua ukubwa wa jamii forum nmeleta hu uzi nikiamini nitasaidiwa..naahidi ataenisaidia nipone kabisa nipo tayari kumfanyia kazi bure mwaka mzima..asanteni sana


Pole sana mkuu, kwanza kabisa ili upambane na Chawa lazima uwe msafi, wewe mkeo na watoto katika nyumba yenu muwe wasafi, kwani mtu mmoja katika nyumba akiwa na chawa ni rahisi sana kuwaambukiza wengine.

Usafi wa nguo, mashuka, nk. Ishitoshe nyoa nywele na nunua kofia na dawa ya kupuliza ya mbu jamii ya expel, pulizia kichwani na vaa hiyo kofia ili kuzuia dawa isipotee, fanya hivyo kwa siku mbili tu kwa watu wote hapo nyumbani.

Kumbuka huwezi kuwa salama na chawa kama siku zote upo karibu sana na mtu mwenye chawa, chawa wanaambukiza.
 
Kijana wa mikoani umefeli wapi?
Umenikumbusha kitambo sana

Anyway..nyoa nywele za sehemu zote. Tena kipara. Chemsha maji ya Moto. Tena sana! Ingiza nguo zako zote,mito,foronya na godoro (kama unavyo). Tafuta dawa ya unga kuua vijidudu (k.v utitiri,kupe,) mwagia chumbani kwako Kila Kona na sehemu.

Mwisho uwe unakoga brother! Na sabuni
hii comment hapan lol,
 
Nyoa nywele zite (upara), na ufanye usafi wa kina ktk kichwa chako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom