GE2025 CHASO yapanga kumfungulia kesi Kiliba wa TAHLISO

GE2025 CHASO yapanga kumfungulia kesi Kiliba wa TAHLISO

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,777
Mwenyekiti wa CHASO (CHADEMA Student Organization) mkoa wa Dar es Salaam Martin Samson Abduli ametoa tamko kwa waandishi wa habari akilalamikia mwenendo wa Rais wa TAHILISO Geofrey Kiliba akidai kuwa unakiuka misingi ya Katiba ya umoja huo wa wanafunzi wa vyuo na vyio vikuu nchini

Akizungumza jijini Dar es Salaam Abduli amesema kuwa Rais wa TAHILISO anatakiwa kutumia majukwaa yake kuzungumzia changamoto zinazowakabili wanafunzi badala ya kujihusisha na siasa za upande wowote au vyama, jambo ambalo linaenda kinyume na Katiba ya umoja huo

"Wanafunzi wanapitia changamoto nyingi kwenye masomo na maisha ya kila siku, hizo ndizo angekuwa anazizungumza badala ya mambo ya kisiasa" -Abduli

Aidha, Abduli amebainisha kuwa tayari mchakato umeanza wa kufungua kesi ya Kikatiba Mahakamani dhidi ya Rais huyo wa TAHILISO, huku akitoa wito kwa wanafunzi kote nchini kuunga mkono jitihada hizo.


 
Back
Top Bottom