CHASO TALK KUFANYIKA MWEZI HUU

May 20, 2015
81
28
Jukwaa la Jumuhia ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanachadema mkoa wa Mwanza yaani Chadema Student Organization (CHASO TALK), inatarajiwa kufanyika mwezi huu. Hili ni jukwaa ambalo huwapa fursa wasomi kutoka vyuo mbalimbali vya mkoa huu kujadili na kubadilishana mawazo. Jukwaa hili hujulikana kama CHASO TALK.

Wanafunzi hawa hukutana na kujadili mambo muhimu yanayo wahusu ikiwa ni pamoja na mstakabali wao wakiwa na baada ya masomo. Inatarajiwa kuwakutanisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya mkoa huo ikiwemo SAUT, chuo cha biashara CBE, chuo kikuu cha tiba Bugando, Chuo cha uvuvi, Chuo cha mipango na Chuo cha Mt. Meru.

CHASO TALK hufanyika katika mfumo wa mdaharo, ambapo mada hujulikana mapema na kuwepo wachokoza mada na baadae washiriki kupata fursa ya kuchangia mada hiyo. Mawasiliano yanafanyika na mda mfupi mgeni rasmi atatangazwa baada ya maandalizi kukamilika.

viongozi mda mfupi watatoa ratiba jina la mgeni rasmi, mada, na siku hasa ya CHASO TALK. Jukumu la kuandaa sasa linashikiliwa na viongozi wa chadema SAUT.
 
Back
Top Bottom