GE2025 Charles Kulwa aomba Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kutupilia mbali pingamizi alilowekewa na mgombea mwezake wa udiwani wa CCM Kata ya Sabasaba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tarimemjini

Member
Joined
Jul 10, 2025
Posts
71
Reaction score
142
Mimi, Charles Andrea Kulwa, nimepokea barua yako leo tarehe 28/08/2025 ukiambatanisha na barua yenye Kumb. Na: RM/INEC/SB/01/25 ya tarehe 28/08/2025 iliyoandikwa na Raymond N. Mwema; ukinitaarifu kuwekewa pingamizi na ndugu Raymond N. Mwema, Mgombea Ufiwani Kata ya Sabasaba kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), kama alivyojitambulisha katika barua yake hiyo.

Napenda kujibu pingamizi hilo nililowekewa na ndugu Raymond N. Mwema, anayejiita Mgombea Ufiwani wa Kata ya Sabasaba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kama ifuatavyo:

  1. Pamoja na mapungufu hayo makubwa, naomba nijibu pingamizi hilo kuwa mimi ni Mwanachama halali wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – Wazalendo), niliyekidhi vigezo na sifa za kuwa Mgombea wa Udiwani katika Kata ya Sabasaba kupitia chama changu cha Alliance for Change and Transparency (ACT – Wazalendo).
  2. Mweka pingamizi, ndugu Raymond N. Mwema (Mgombea Udiwani wa Kata ya Sabasaba kupitia Chama cha Mapinduzi – CCM), sababu alizotumia kuniwekea pingamizi hazijitoshelezi.
  3. Kwanza, napenda ukubaliane nami kuwa katika mchakato huu wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025, hakuna nafasi ya Mgombea Ufiwani. Na kwamba kwenye Ofisi yako huna wagombea wa nafasi ya Ufiwani kama anavyojiita ndugu Raymond N. Mwema; isipokuwa kuna Wagombea Udiwani Kata ya Sabasaba. Ama yawezekana kuna uchaguzi mwingine unaoendelea wenye nafasi hiyo anayoitambua ndugu Raymond N. Mwema anayoigombea yeye.
  4. Uhalali huo unatokana na pale nilipoamua kuachama na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama kingine c...
 
Ufiwani ndiyo inamaanisha nini. Ingekuwa mgombea wa ACT ndiyo kaandika maneno hayo ufiwani angefutiliwa mbali.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…