Chanzo cha wanaume kufa mapema

Chanzo cha wanaume kufa mapema

yuda75

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
520
Reaction score
1,403
*

Nimefundisha semina nyingi za wajane 99.9% wanaohudhuria ni wanawake. Mchango huu hapa chini una ukweli usiofichika.
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
SABABU INAYOFANYA WABABA KUFA MAPEMA!!

Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini huwa anakua na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake, familia humsikiliza, huzingatia uwepo wake!

Tatizo huanza pale baba anapozeeka, nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, amestaafu! Na pale watoto wanapokua wamekua watu wazima wameanza maisha yao! Hapo ndipo mambo kwa baba humgeuka!

Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa huanza kupungua taratiib.. baba hasikilizwi tena Kama zamani, isitoshe anakua hahusishwi sana tena kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa atasaidia nini na pesa hana? Badala yake mkewe huanza kuwafanya watoto kuwa washirika wake zaidi na kumuweka kando mumewe... Baba anaachwa pembeni!

Mama huanza safari kwenda kwa watoto, huko hukaa sana, baba kaachwa nyumbani peke yake! Watoto wanagombea mama aende kwao, lkn baba hakuna anayemtaka!

Wakiwa nyumbani na mkewe, simu toka kwa watoto 80% anapigiwa mama, baada ya maongez mareefu, ndo baba anapewa simu anasalimiwa dk 2 imeisha hiyo! Baba simu anayo, ila haoni simu za watoto wakimpigia, na wakimpigia ni kwa sababu maalumu tena maongez huwa mafupi! Hawana muda nae!

Baba anajikuta anakuwa mpweke sana, anakua mgeni kwa familia yake mwenyewe! Wale ambao alizimalizia nguvu zake za ujana kuwatafutia hawana muda nae!

Pale baba anapokuwa anaihitaji sana faraja ya familia yake sababu ameshazeeka... Familia humpa kisogo! Upweke unamsonga! Sababu ya upweke mawazo humsonga, hili hupelekea kinga ya mwili kushuka na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na magonjwa na haichukui muda anafariki!

Familia wataliaa, watachapisha matisheti, watatoa mapesa kumnunulia sanduku la gharama na kumjengea kaburi la gharama, mitandaoni watampost sana! Lakini alipokuwa hai... No one cares!

Tuwajali baba zetu, walijitoa na kujinyima sana kufanya tufike tuliko! Ni dhambi mbele za Mungu tena ni laana mbaya kuwapuuza baba zetu!

Wakati unaendelea kumsifia mama yako kuwa ni bora, msifie hata baba kwa kukuchagulia mama aliye bora.๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚
 
Umesema kweli
Ila wababa wako serious sana yaani wengi hawanaga story hadi watoto wanawaogopa maongezi yetu maranyingi ni salamu tu na kuomba hela za shule
Mapenzi ya kweli yapo kwenye kuspend time together ndio maana tunawajali na kuwakumbuka mama zetu na kuwasahau wanaotupambania tule
Wababa tubadilike hata kama unafanya kazi ngumu unarudi umechoka tumia muda wako japo kidogo piga story na watoto inakuza mapenzi kuliko kuwapa hela ya shule kila siku
 
Umesema kweli
Ila wababa wako serious sana yaani wengi hawanaga story hadi watoto wanawaogopa maongezi yetu maranyingi ni salamu tu na kuomba hela za shule
Mapenzi ya kweli yapo kwenye kuspend time together ndio maana tunawajali na kuwakumbuka mama zetu na kuwasahau wanaotupambania tule
Wababa tubadilike hata kama unafanya kazi ngumu unarudi umechoka tumia muda wako japo kidogo piga story na watoto inakuza mapenzi kuliko kuwapa hela ya shule kila siku
Tutajitahidi
 
Hili huwaga nalihis his sometimes kuwa huenda wife anaweza kuniletea hiz pigo maana dahh!!!.
Ngoja nianze tiz mapema nisizeeke kiboya unakua mzembe mzembe.

NB.
mwanaume usiwategemee sana (kama sio kabisa) wanao.jiandalie mkakati mapema wa ku survive bila wao (msaada wao wala kampani yao) utakapo kuwa nguvu hazitoshi
 
Sababu nyingine inayosemwa ni kwamba wanaume ni watu wakuweka machungu moyoni bila kusema, sasa hii hali unakuta inaleta mawazo na kuathiri afya taratibu taratibu ndio baadaye athari inaonekana. Wanawake kwa kawaida hawaifadhi machungu moyoni.
 
Ulichokieleza huenda ikawa ni moja ya sababu lkn pia usisahau wakina baba huanza kufa kabla ya wakina mama kutokana na mambo yao ya kuhatarisha afya, mfano pombe, sigara, ufuska, kutokupata muda wa kupumzika n.k.
 
Back
Top Bottom