Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
Hili linaweza kuwa somo gumu hata kwangu mtoa mada,lakini nitajitahidi kueleza kadiri ya uwezo wangu
Wakati Mungu anatukataza tusile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya,huenda Mungu alikua na maana kubwa sana kwetu wanadamu
Ni muda mrefu sasa nimekua nikitafakari ni nini lengo la Mungu kutaka tusijitambue,nilichokigundua kutoka kwenye tafakari yangu ndo leo nimeona nije hapa ili niongeze majibu lakini pia niwajuze kile nilicho kigundua lakini zaidi sana mnikosoe,hii naamini ndio njia nzuri ya kujifunza
Nimegundua kuwa KUJUA ndio chanzo cha ubaya na uovu wote
KUJUA ninakokuzungumzia ni kupata ufaham wa yale uliyokua huyajui,mfano;
NIKIJUA ulipoweka fedha zako nitakuibi kirahisi sana
Wanadamu tulipopata KUJUA namna mwili wa binadamu unavyofanya kazi ndipo watu wametengeneza sumu na silaha mbalimbali ili kumuangamiza binadamu mwenzao
Nchi jirani ITAKAPOJUA siri ya nchi nyingine,chi hiyo usalama wake unakua mashakani
Hata jirani yako ANAPOJUA siri zako,unakuwa na mashaka
Mifano ni mingi sana lakini ukitafakari ujagundua kuwa,KUJUA kuna faida na hasara,lakini inaonekana hasara ni nyingi ukilinganisha na faida
Sijui kama nimeeleweka kile ambacho nasema hapa lakini mpaka sasa naamini binadamu amekua mhanga mkubwa sana wa KUJUA au UFAHAMU
Hapa ndipo ninapoiona sababu ya Mungu kutuzuia KUJUA au kupata UFAHAMU,inaonekana hatuna uwezo wa kuwa na UFAHAMU kwa kuwa umetuletea maumivu badala ya nafuu,hatukutakiwa tuwe na UFAHAMU kabisa
Hapa ndipo napata ujasiri wa kusema,KUJUA au UFAHAMU ndio chanzo cha uovu wote duniani
Wewe unasemaje?