Chanzo cha ufisadi na dawa yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanzo cha ufisadi na dawa yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by pay2play, Jan 14, 2009.

 1. p

  pay2play New Member

  #1
  Jan 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wengi wamekuwa wanajiuliza ni kwa nini sasa kuna ufisadi sana kuliko miaka ya nyuma,wengi wa viongozi wamekuwa matajiri katika kipindi kifupi sana,uku wakiacha wananchi walio wengi katika umasikini mkubwa wa kupindukia.chanzo kikubwa sana cha ufisadi kilianza miaka ya 1993 baada ya TZ kubinafisisha viwanda na mashirika ya umma,baadhi ya viwanda na mashirika ya umma yalikuwa yakipata faida kubwa sana,waliyauza kwa bei ya dezo na mengine kujipa wenyewe,mpaka kufikia juni 2003 Tanzania ilikuwa imewauzia au kuwapa kwa ubwete viwanda na mashirika ya umma 309 watu binafsi au wawekezaji wa kigeni uku 10% zikimwagwa au kuwa wamiliki wa kimya kimya,mfano Tanzania breweries,Tanzania cigarette,Tanga,Twiga,na mbeya cement.
  Baada ya kuwa hakuna vyanzo vya wizi kwani vyote vilikuwa vimeuzwa au kupewa baadhi ya viongozi ndipo wengi wa viongozi walipanza kuanza kuanza ufisadi au madili ya Tenda,wizi wa fedha,nk kiasi cha kufanya Nchi kutokuwa na kitu chochote kile kwani watu walionunua walikuwa wanalipa kodi ndogo sana au kutokulipa kabisa .
  Ili kuuzima ufisadi na kuukomesha itabidi tujue Mashirika na viwanda zaidi ya 400 kila moja yaliuzwa kiasi gani?kwa nani?je wanunuzi wanalipa kiasi gani ya kodi,pesa ya mashilika zimetumika vipi?hapo ndipo tutawagundua wabaya wetu.
  Naomba msifanye utani tuchunguze jambo ili kwa makini ili tuwakomboe wabongo ambao wako kwenye dibwi kubwa sana la umasikini wa kutupwa.
   
 2. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  it is seroius, I agree with pay2play
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Dawa ya ufisadi ni kurudisha Azimio la Arusha,maadili ya viongozi wa umma na kutenganisha biashara na siasa.Utendaji uwe wazi serikalini na kwenye taasisi zake ili kuzuia kuficha uovu,mikataba yote iwe wazi ili kuzuia ujanja ujanja kutandeka.
   
Loading...