Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,277
- 2,933
ni kama mwenzi mmoja umepita tu nlikuwa na wenzangu kadhaa tunajaribu kuinusuru ndoa ya jamaa yetu ambayo ilifungwa miezi 4 iliyopita. imagine miezi 4 tu tena wao wanasema ni mingi sana..wameamua kuachana. ilikuwa ni kazi ngumu sana. siku hiyo tumekaa kuanzia saa kumi jioni moaka saa tisa usiku tunawasihi sana kuwa wasichukue uamuzi huo. si mwanamke si mwanaume wanasema kila mtu ashike hamsini zake na njia yake.
iliniuma nikikumbuka namna tulivyohangaika sana kwa ajili ya harusi ile ya kifahari ya jamaa yetu.walipendeza sana wakisifiwa na kila mtu. miezi miwili hawataki hata kutizamana.kila mtu anaona kama alioa ua kuolewa na shetani.nikarudi nyumbani saa 10 hivi nikiwa nimechoka sana nikakaa tu sebuleni mke wangu akanifuata na kuniuliza kulikoni huko.
machozi yakinitoka nilimweleza x na y wameamua kabisa kuachana. wazaz wao walishakaa nao, viongozi wa dini walsihakaa nao,wazee mbalimbali walishakaa nao.wameshikilia msimamo huo.hakuna anayetaka kujishusha... kila mtu anasema ana uwezo mzuri wa kuishi bila mwenzie.
nlisikitika sana..nlipata neno la kujifunza.nlimtimzama mke wangu sana akiwa amekaa kwenye kochi.sikutaka kuwaza kati yao nani ana makosa. sababu lengo kubwa la tuki lile lilikuwa ni kusuluhisha....sikulala.asubuh sana saa moja jumamosi nikaenda tena nyumban kwao. nilimkuta x amelala sebulen kwenye sofa na mkewe akiwa chumbani. nlimwomba shemeji yangu aje sebuleni baada ya kama dk 20 akawa amefika.
jamaa yangu aliamka akapiga mswaki akarudi tukakaa wote tukiwa hatujui cha kuzungumza.nlikaa tu natizama chini nao wakitizama sehemu walizojua wao. mle ndani kulikuwa kimya sana.hatukuwasha radio wala tv. kulikuwa kimya sana. tuliendelea kukaa vile kwa muda mrefu kiasi. mwishoni nikamwambia mke aanze kuongea tatizo la mumewe ni nini. aliongea mengi sana aliongea mpaka akalia....nikashukuru moyoni kwa hilo.
mwanaume nlimwambia asijibu hata kidogo. kwa lolote ambalo ameongea mke wake yeye anyamaze iwe kweli au si kweli. baadaye aliposema "shem mi nimemaliza" nikamwambia mwanaume asijibu zile hoja. ila naye aleze tatizo ni nini. alizungumza yake mengi pia akafikia akasema amemaliza. nikawaambia kwa kila mtu ambayo ameyasikia kutoka kwa mwenzie aanze kuyatafakari.si kuyapangua,au kujitetea.ayatafakari tu. pia wakumbuke walishakuwa pamoja kwa muda kabla ya kuamua kuoana. je hayakuwepo hayo?kama hayakuwepo kwa nini sasa yapo?
ule ugomvi uliisha..mke akaomba sasa arudi kwao kwa week moja akapumzike then atarudi kwa mumewe waendelee kuishi. mume akaridhia mwanamke akachukua nguo chache tu tofaut na mwanzo alikuwa amefunga kila kitu chake. nlikaa nao mchana tukatoka kwenda kula home kwangu. tukajikuta tumefikia hatua ule ugomvi umekuwa ni utani sasa nao wakitaniana kila mmoja anamwambia angemwacha mwenzie asingepata kama yeye..kwa utani na kicheko. yule dada hakwenda hata kwao tukawa wote mpaka usiku saa tano nikawarudisha kwao...nikawaambia walale wote chumbani ila walale mzungu wa 4 na hamna kugusana..walicheka na yakaisha walilala wakawa mke na mume tena. ni week kadhaa zimepita,
NINI TATIZO LA NDOA ZETU VIJANA? KWA WAKE NA WANAUME TUNAOCHAGUA WENYEWE?