Huwa kuna parental stock ambao wanakuwa special kwa ajili ya kutaga mayai tu. Kama parental stock ni kwa ajili ya nyama basi mayai ambayo ni makubwa yakishatagwa ndio huwekwa katika mashine tayari kwa kutotolewa. Hii itapelekea kupata vifaranga wakubwa ambao wengi wanakuwa ni majogoo. Na kwa wale wa mayai nao ni hivyo hivyo, lakini si kweli kuwa eti wanatotolewa majike tu. Wakishatotolewa huchaguliwa wale wenye dalili za kuwa majike na ndio huuzwa. Majogoo hutunzwa kwa kuuzwa kama mabroilers.
Nina uzoefu na hii kazi na nimewahi ifanya, hawa broilers hawajatokea tu wana wazazi....