Channel za star times vipi? Msaada

Channel za star times vipi? Msaada

iryn alphonce

Member
Joined
May 15, 2014
Posts
49
Reaction score
8
Baadhi za channel za star times zinaandika no service na hazionyeshi kitu,msaada nifanyeje ili ziwe kawaida
 
Kiukweli hiyo kampuni ya wachina kwa sasa inabore sana.

Mimi pia nina king'amuzi cha startimes, kwa siku kadhaa sasa TV yangu kwenye channel nyingi, aidha itaandika no srrvice na kwenye zile channel ambazo angalau zitakuwa zinaonekana, basi ni scratches kibao!

Hiyo kampuni wakati wanafunga mtambo wao hapo Makongo, si walituassure sisi wateja wao kuwa sasa tatizo la kutoonekana vizuri channel, kwa wanaotumia ving'amuzi vya startimes, itakuwa imefika mwisho.

Mbona sasa badala ya kuimprove, mambo ndiyo yamekuwa more worse, sisi wateja tunatuma salaam kwenu startlimes, hizi ni zama za free market, kama hamtataka kuboresha huduma yenu, sisi wateja hatutakuwa na option nyingine zaidi ya kuwakimbia na kuhamia kwenye ving'amuzi vingine.
 
Inawezekana sisi TZ wakati wa kutoka analogy na kuhamia dijitali ulikuwa haujafika, lakini kwa kuwa ving'amuzi ni dili za watawala wetu kama siku za nyuma waTZ wenye mabasi walivyolazimishwa kununua speed governors, ndizo hizi kero tunazozipata za kuzungusha milingoti ya antenna hadi basi na bado tunashudia kitu kinachoandikwa no service kwenye luninga zetu au scratches kibao!
 
Hamna usipolipia ndio inaleta mawenge hyo alaf nw kila station inabid ulipie hamna cha local wala nn yaaaan mmbo ya bure yameisha sasa hvi cha bure jua na mwez tu
 
King'amuzi gani kinaganda toka asubuhi mpaka jioni?
 
labda nyie wa dar ndo mnakutana na hizo.cc huku arusha mbona poa tu channels tunazipata vzr bila tabu.scrach zinasababishwa na antenna yako.jaribu kutumia hata ile antena ya nje ndefu ttz lako litakwisha.pia angalia pia plug ya cable ya antena nyuma unapochomekea kwenye king'amuzi kama iko sawa.
kama ukifanya yote hayo na ttz likawa bado wasiliana nao.lkn huku kwetu hatuna matatizo hayo kbx.na chanels za free zipo kama kawa
.
 
Back
Top Bottom