kibaizi kiki
Senior Member
- Dec 23, 2012
- 160
- 38
Kampuni hii imekuwa kwenye utangazaji wa tv kwa muda mrefu sasa. Lakini pamoja na uwezo mkubwa ya kuyafikia maeneo mengi na kutoa taarifa nzuri kwa watanzania, wana tatizo la kutokuandika majina ya watu wanaowaonyesha aidha wakati wakiwahoji ama kuchukua habari zao. Kama mtazamaji umeikuta taarifa ya habari katikati basi hutaweza kujua anayehojiwa wala jina la picha inayooneshwa. Sina uhakika kama ni mtaalamu wa graphics ndio anatakiwa lakini nina uhakika ni jambo lipo ndani ya uwezo wao kwani mara moja moja uandika majina. Tafadhali, Channel 10 boresha hilo kwani lina umuhimu wake kwenye habari