Channel 10: Francis Godwin ateta, nusura auawe

BASHADA

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
513
148
Kipindi cha Hamza Kasongo, mwandishi wa Iringa na makamu wa IPC na mmiliki wa blogu ya francisgodwin ametoa ushahidi kuwa alikuwa akijaribu kupiga picha baada ya Mwangosi kuuawa, polisi wakamnyooshea bunduki akakimbia akapotelea porini msituni. Aliporudi akachukuliwa na dereva wake, akawa anafuatwa na magari mawili kila anapoenda, mwishowe akaingia uchochoro fulani akawapiga chenga alafu akapiga simu redioni kuwajulisha kuwa yuko mochuari ili kuwapoteza polisi ndo pona yake, huenda na yeye angekuwa marehemu.

Update: anasema alitokea msitu wa Sao Hill, dereva wake akamwambia wanakutafuta. Salama yako ondoa label zilizobandikwa kwenye ubavu wa gari ili wasijue kama gari la mwandishi wa habari, wakaondoka ndo wakaanza kufukuziwa. Wakiongeza mwendo jamaa wanaongeza, wakipunguza nao wanapunguza, wakiingia sehemu nao wanaingia. Bila shaka kuna jambo hapo wadau
 
Mtabisha nini mkiambiwa policcm ndiyo waliotaka kumuua Ulimboka na bado wanaendeleza mkakati wao? Hivi mmeshajiuliza wametumwa na nani? mnadhani wanafanya tu? naona the Hague ikinukia! muda si mrefu, shetani anazidi kuwafumba mamcho waue zaidi ili hukumu iwe kubwa zaidi
 
Nafikiri siku hiyo walitumwa kuua waandishi wa habari. Next time sijui itakuwa nani.... tusipowadhibiti hawa watatufuata hata majumbani mwetu. Nasema tena na tena mbona mashahidi wako wengi tu tume ya nini?
 
Dah...alifanikiwa kukimbia na camera yake? Maana ni muhimu sana picha zake zikitumika baadaye kama ushahidi
 
Samahanini ma greatthinker kwa kusema haya lkn ndio ukweli huu.

M4C inamanisha ina lengo la kubadilisha utawala si ndio? nahic jibu ni ndio..sasa kama ni hivyo maafa ndio gharama yake so kama kweli nia ni kwenda ikulu basi wahusika muwe tayari kwa hayo maana hakuna atakayeachia madaraka kirahic...kama M4C hawezi kujitoa kwa haya yanayotokea basi bora iache mara moja na kukubali tutawaliwe vyovyote tunavyokwenda.

Ila wote M4C na watawala tukumbuke hapa ni duniani kuna maisha kwa mungu tunayemuamini lbd kama ninyi hammuamini mungu-ni hayo tusipige porojo sn.
 
Kwa dr ulimboka walificha ushahidi kwa mwandishi wa habari hadi picha zipo na bado wanakataa
 
Mkuu ameongea kwa kifupi ila inaonekana hawakufanikiwa kumpora camera, jamaa anaongea kwa uchungu sana. Anyway kipindi kimeisha
 
Police wanatangaza vita tanzania bila kujijua, wanasahau wengi wao wanaishi mtaani, haya mambo wanayofanya yatawatokea puani, wanadanganya mchana kweupe, wanabishana na picha za matukio,bila shaka wataanza kukataa vivuli vyao.
 
Kipindi cha Hamza Kasongo, mwandishi wa Iringa na makamu wa IPC na mmiliki wa blogu ya francisgodwin ametoa ushahidi kuwa alikuwa akijaribu kupiga picha baada ya mwangosi kuuawa, polisi wakamnyooshea bunduki akakimbia akapotelea porini msituni. Aliporudi akachukuliwa na dereva wake, akawa anafuatwa na magari mawili kila anapoenda, mwishowe akaingia uchochoro fulani akawapiga chenga alafu akapiga cm redioni kuwajulisha kuwa yuko mochuari ili kuwapoteza polisi ndo pona yake, huenda na yeye angekuwa marehemu update: anasema alitokea msitu wa sao hill, dereva wake akamwambia wanakutafuta. Salama yako ondoa label zilizobandikwa kwenye ubavu wa gari ili wasijue kama gari la mwandishi wa habari, wakaondoka ndo wakaanza kufukuziwa. Wakiongeza mwendo jamaa wanaongeza, wakipunguza nao wanapunguza, wakiingia sehemu nao wanaingia. Bila shaka kuna jambo hapo wadau

Duh!!!,,kama Somalia vile.Halafu kiongozi wa nchi anasimama na kupaza sauti kwa wananchi kuwa"Tanzania pana amani/sio nchi ya vita/raia wake wana mahusiano mazuri dhidi ya Serikali yao"IPO SIKU SERIKALI MTAYALIPIA HAYA MATAMKO.
 
Mkuu figganigga, ni kwamba alipopiga cm kwenye vituo vya redio na kuwapa taarifa kuwa kwa sasa yuko hospitali ameenda kuangalia mwili wa marehemu na redio ilivyorusha hewani wakapigwa chenga ya mwili
 
Back
Top Bottom