Chanjo ya tatu ya COVID-19 yapata mafanikio

Chanjo ya tatu ya COVID-19 yapata mafanikio

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,378
Chanjo dhidi ya virusi vya corona inayotengenezwa na kampuni ya dawa nchini Uingereza ya AstraZeneca na chuo kikuu cha Oxford imepata mafanikio makubwa katika hatua ya majaribio na sasa iko tayari kuanza kutumika.

Hayo ni kulingana na mkuu wa kampuni ya AstraZeneca katika mahojiano na gazeti la Sunday Times ambaye amesema chanjo hiyo inaweza kutoa kinga kwa asilimia 100 dhidi ya COVID-19 baada ya mtu kupatiwa dozi mbili.

Chanjo hiyo ambayo sasa inafanyiwa tathmini na taasisi ya udhibiti wa dawa nchini Uingereza ina ubora sawa na zile ya kampuni za Pfizer-BioNTech na Moderna ambazo tayari zimeanza kutumika.

Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Telegraph chanjo ya AstraZeneca inaweza kupatiwa ithibati kesho Jumatatu na tayari serikali ya Uingereza imeagiza dozi milioni 100 zinakazotolewa kwa mamilioni ya watu nchini humo.
 
Hao ndio wasomi waliosoma wakaelimika. Elimu ya kuwinda teuzi badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kijamii ni bure.
 
Vitu vingine hovyo Sana. Yaani inatolewa chanjo ambayo hata haielezi athari zake upande mwingine Kama mtu zikimkataa maana binadamu tumepishana Mambo mengi mpaka magroup ya damu. Asante Mr President John Pombe Magufuli kwa kuwa na fikra pevu iliyovuka fikra za Walimwengu wengi.
 
Kifupi binadamu milioni 100 wanaenda kuambukizwa kovidi isiyokuwa na madhara. Au yenye madhara kwa upande mwingine unaofichwa
 
Hao ndio wasomi waliosoma wakaelimika. Elimu ya kuwinda teuzi badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kijamii ni bure.
Ni kweli kabisa kuna wale wengine wanajiita wapigania hadi ila haki yenyewe wanaidaia mitandaoni tu huku wameficha utambulisho wao, yani kuna watu ni bure kabisa.
 
Hao ndio wasomi waliosoma wakaelimika. Elimu ya kuwinda teuzi badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kijamii ni bure.
Hapa kwetu ukiteuliwa ndipo unapata fursa ya kutatua matatizi ya jamii:
Mrembo akiteuliwa anaweza kupunguza zeros katika wilaya.

Asiye na kazi akiteuliwa anaweza kifufua magari yaliyotelekezwa.

Wengine eakiteuliwa wanaeeza kupromote utalii wa ndani kwa kutumia wasanii
 
Back
Top Bottom