Change is Possible

Change is Possible

Tujisahihishe Tz

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2011
Posts
3,061
Reaction score
1,367
ufika mbali ikiwa jitihada mahsusi zitawekwa
ili watu wa Taifa hili watoke hapa tulipo. Katika
maisha yangu yote nimeendelea kuamini toka
nilipopata akili zangu katika uwezo wa Taifa hili
kukua na kutoka hapa tulipo. Kwanini tusifanikiwe kama tukiamua kwa dhati kuleta
mageuzi katika nchi yetu? Mabadiliko
yanawezekana ni maamuzi yetu tu ya dhati. Kama Taifa kamwe hatutakuwa na furaha kama
hatutawekeza juhudi zetu kuleta mageuzi
katika Taifa hili. Tutakuwa na furaha kama tukiwa na mipango
ya pamoja kisha kuwekeza fikra na nguvu zetu
kufanikisha mipango hiyo. Taifa hili ni Taifa la
watu wasiokuwa na furaha kwasababu kama
Taifa hatujafanikiwa kitu chochote kikubwa cha
kujivunia. Ni muhimu kuwekeza juhudi zetu ili kuandika historia katika dunia. Na hili
hatutafanikiwa kama hatutakuwa wamoja
kama Taifa. Ni muhimu kutambua hili, tuna kitu
cha kukijenga kama watu tunaoishi pamoja.
Kitu hicho ni nchi yetu. Tukiijenga nchi yetu
vizuri tutajivunia. Lakini hatutaweza kuijenga vyema nchi hii pasipo kwanza kujenga
mahusiano yetu. Kama tutapendana sisi wenyewe kwa wenyewe
tutakuwa na nafasi kubwa ya kulijenga Taifa
hili. Ni lazima tulipende Taifa hili ama sivyo
hatutakuwa na nguvu ya kulijenga. Kwahiyo
lazima tuelewe hapa ni sehemu pekee ambako
tunaweza kupaita nyumbani. Kwahiyo ni lazima juhudi mahsusi zifanyike kuwaleta watu pamoja
ili tulijenge Taifa hili kwa pamoja. Najua kuna matatizo ya corrupt leaders ambao
ndio chanzo cha mgawanyiko uliopo. Lazima
tuwaambie ukweli. Kwamba wana haribu
mwelekeo wa Taifa hili na future yake. Lazima
waelewe wao wamekuwa viongozi kwa lengo
moja tu, kuleta umoja wa watu wa Taifa hili na kulitoa Taifa hili kutoka hapa lilipo. Lazima
wajue cheo ni dhamana na wana majukumu ya
dhati ya kulijenga hili Taifa na sio kinyume
chake. Roho ya uzalendo ya watu wetu
imepotea sababu yao. Ni lazima wajue historia
itawahukumu. Watazania wana kiu ya kusonga mbele kama Taifa na hili halitowezekana kama
tusipokuwa wamoja. Taifa limekosa uongozi
wenye maono na hili ni Tatizo kubwa sana
ambalo naliona. Naona msambaratiko katika
familia, katika dini na katika ukabila. Hivi vitu
vyote vinahitaji kuunganishwa na kuwa kitu kimoja. Ili tujenge Taifa imara. Wajibu wa mtu
kwa familia yake, kwa jamii yake na kwa Taifa
lake. Sisi sote tuko pamoja katika ujenzi wa
Taifa hili. Kama ni nyumba tunatakiwa
tuinyanyue pamoja na kuiezeka pamoja. Tukifikiria au tukiwa na fikra ya kwamba
uongozi ni sehemu ya kupatia mali au
kutajirikia tutakuwa hatulipendi Taifa hili na
baadae yetu itakuwa matatani. Muono huo
ambao uko akilini mwa viongozi wengi ni hatari
kwa uhuru na mustakabali wa watu wa Tanzania. Uongozi sio sehemu ya kutafutia
ufahari au sifa. Uongozi ni kitu kingine kabisa
na unahitaji mtu mwenye maono na mwenye
busara kwakuwa unahusiana na uhuru na
maisha ya watu, una husiana na haki za watu.
Ukiwa na Taifa la viongozi wa namna hiyo nchi haitokalika na haki haito tamalaki. Taifa
huunganishwa kwa haki. Order na harmony
katika Taifa italetwa na haki tu. Tutakuwa na Taifa lenye watu ambao
watakuwa wanagombania kama fisi Mali ya
Taifa, tutakuwa na vurugu na fujo na maskini
hawatopata chochote, tukiwa na viongozi
walifuata mali katika siasa haki itatendekaje?
Tunahitaji kiongozi atakaye tufikisha salama katika safari yetu. Kiongozi huyo sio mwingine
bali ni mwenye busara na maono. Msidhani DRC imelaaniwa na Tanzania
itaendelee kubarikiwa ikiwa Viongozi wetu
wataendelea kuabudu mali. Hatua ya kwanza
ya serikali yeyote kuwa ya kiimla ni pale
inapoanza kuwa ya kifisadi na yenye tamaa ya
mali. Ni lazima itagandamiza watu wake. Kubadilisha mawazo kutoka kutumikia watu
kuja kujilimbikizia mali ni hatua ya kwanza ya
ugandamizaji dhidi ya raia. Wananchi wana haki
ya kulinda uhuru wao dhidi ya serikali yeyote
ya kidhalimu ambayo haizingatii maslahi ya
umma. Kwahiyo kundi dogo litahodhi utajiri na kujikusanyia mamlaka na kudhani ya kwamba
wana haki ya kutawala wengine, uongozi
utakuwa wa kuridhishana. Kutakuwa na
maskini wengi mno na matajiri wachache. Watanzania ni lazima wafikirie upya uhuru wao
ambao kwasasa unaonekana uko mashakani
au umewekwa reheni na kikundi kidogo cha
watu kilicho hodhi utajiri mkubwa usio halali,
kundi hilo ni la viongozi. Watanzania wana haki
juu ya bunge, mahakama na serikali. Ambavyo vyote vinaonekana viko corrupt. Na imani ya
wananchi juu ya vyombo hivyo ni ndogo. Raia
wowote wale popote pale duniani wana haki ya
kuiondoa serikali yeyote iie isiyo kidhi matarajio
yao na matumaini yao ya kujenga jamii huru na
yenye matumaini. Watu wa Taifa hili wana hamu ya maendeleo lakini wanazuiwa na rushwa na
viongozi waliokosa dira na will power ya
kulinyanyua Taifa hili kutoka hapa lilipo. Nchi hii kamwe haitojengwa kwa propaganda
na uongo bali itajengwa kwa haki na ukweli.
Nchi hii haitojengwa kwa porojo bali kwa
juhudi za dhati za watu wake kujiletea
maendeleo yao wenyewe. Ni ukweli
usiopingika kuna upuuzi mwingi unaendelea katika Taifa hili ambao hauvumliki kwa mtu
ambaye ana hamu ya kuliona Taifa hili
likinyanyuka. Vijana wa Taifa hili wanahitaji
kuona Taifa hili likiendelea. Hatutuwezi
kuendelea na viongozi waliopo. Lazima uje wito
mpya katika Taifa hili wa uongozi na uadilifu. Vijana wa Taifa hili lazima wajengwe upya
kulipenda Taifa lao ni wao tu wenye uwezo wa
kulinyanyua Taifa hili kutoka hapa lilipo. Vijana
wa Taifa hili wanahitaji heshima kwa Taifa lao.
Hatuwezi kuendelea kujenga Taifa hili kwa
porojo. Lazima tulijenge Taifa hili kwa akili na ukweli. Raia wana haki ya kuambiwa ukweli
kuhusu nchi yao. Ni lazima tujenge msingi mpya wa Taifa hili na
tusonge mbele. Hatutaweza kama hatutakuwa
wamoja katika akili na roho. Hatutaweza kama
hatutajenga uaminifu na kuheshimiana
miongoni mwetu. Kila wakati nimekuwa nikiamini hatua ya
kwanza kwa Taifa lolote kupiga hatua ki
maendeleo ni kwa raia wao kulipenda Taifa lao.
Ni lazima tulipende Taifa letu. Ni lazima tuzalishe
watu wetu bora ambao watetembea kifua
mbele duniani kote. Hili lazima litokee na hii ndio itakuwa furaha yetu. Sisi kama Taifa ni
lazima tukue. Kuna chaguzi mbili tu. Tukubali na
kutia juhudi kufanikisha ndoto yetu ya kwamba
tuna uwezo wa kuwa Taifa kubwa kama
tukijipanga na kutia juhudi au tusiamini na
tubaki hapa tulipo kwenye udhaifu wetu? ”This need bold decision and courage” but we must
move forward like trained Army. We must move
forward. We have the power to move this
Nation forward. Hatuwezi kuendelea kuwa
watu wanaotafuta kwenda kupata mali kwenye
uongozi. Tunahitaji viongozi watakao lisongesha Taifa hili. Those who will uplift the
spirit of the ”Nation”. We must have our core ”
beliefs” . Tuna viongozi ambao they lead us no
where. Watu wa taifa hili wanahitaji muongozo
na dira. Wanahitaji jua la asubuhi liwamulikie na
matumaini yawajae mioyoni mwao. Tumaini ambalo litajenga Taifa hili. Tunahiaji viongozi
wanaoamini kwamba Taifa hili lazima lisonge
mbali kwa damu na kwa jasho. Tukiwa wamoja
nothing shall be impossible to us. Tunahitaji
kongozi atakayeanzisha movement hii.
Kiongozi mkweli na mzalendo. We must build spirit of love and admiration
toward this country. Our children must love this
NATION. We have ability to grow and to become
greater kuna msemo ambao tunauzungumza
sana; ”Hata mbuyu ulianza kama mchicha” .
There is the truth on this. Kama tukiamua leo kwa dhati kabisa za nafsi zetu kulijenga Taifa
hili nani atatuzuia kuwa Taifa kubwa? Ni juhudi
zetu tu na umoja wetu na uaminifu katika
kulijenga TAIFA hili. Taifa lolote litakuwa huru
pale litakapo jitambua na watu wake
watakapojitambua, ni lazima tujitambue sasa. Those who are educated must initiate change
and growth. Ni lazima tujenge watoto wetu katika utaifa na
katika uzalendo. Ni lazima waamini katika
Utanzania.’Tutakapo badilisha mawazo ya watu
kutoka katika ubinafsi kuja kwenye utaifa ni
hatua ya kwanza ya maendeleo. We need honest leaders who speaks from their
hearts, who are ready to sacrifice everything for
the Nation growth.We need a leader who will
move our cause forward. We must set a Nation
dream and handover that dream in each
generation. I want you to believe this; our
 
Nimeikubali hii Mkuu, naenda kuapply popote nitakapokuwa. Na lazima matunda yaonekane. Kila mwenye kiu ya maendeleo vision kwa ajili ya Taifa letu hapa kuna kitu cha kuchukua
 
Back
Top Bottom