Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,532
- 34,910
Kilimo cha umwagiliaji na changamoto zake
Wote tunajua kwa sasa tunakabiliwa na upungufu mvua na kutotabirika kwa mvua! tumekua tunategemea kilimo cha mvua, na kwa hali ilivyo tukiendelea kutegemea mvua ni Dhahiri kwamba NJAA itabisha hodi milangoni mwetu! Suluhisho la kilimo kwa sasa ni kufanya kilimo cha umwagiliaji ambacho kwa namna moja au nyingine kinakabiliwa na changamoto mbali mbali hasa kwa nchi kama Tanzania!
Zifuatazo ni baadhi ya changamoto zinazokabili kilimo cha umwagiliaji Tanzania:
1. Mtaji na vyanzo vya mitaji (funds/capital).
Ili uweze kufanya kilimo cha kisasa utahitaji vifaa kama pampu, mipira, na vifaa vingine ambavyo kwa pamoja vinahiji mkulima awe na uwezo kuvimudu! Huwezi kufanya umwagiliaji wa matone (drip irrigation) kama huna uwezo kifedha kitu ambacho mkulima wa kawaida kijijini hana! Pia vifaa vingi vya umwagiliaji vinauzwa makampuni kwa bei ambayo sio rafiki kwa mkulima wa kawaida.
2. Upungufu wa maji na utowekaji wa vyanzo maji.
Hii inatokana na mabadiliko ya tabia ya nchi. Juzi juzi tumeona mto ruvu umepungua maji, mabwawa pia maji yamepungua, chem chem zilizokua zinatoa maji nazo zimekauka! Tunajua maji ni kama injini katika kilimo cha umwagiliaji na kama hamna vyanzo maji vya kutosha ni Dhahiri kilimo cha umwagiliaji hakitafanikiwa!
3. Ubora wa nyenzo za umwagiliaji.
Kuna wimbi la vifaa visivyo na ubora katika soko la Tanzania, hali hii inapelekea mkulima kununua bidhaa kama pampu (ambazo zinagharama kubwa na zinahitaji mtaji mkubwa) zenye kiwango duni hali inayopelekea mkulima kuingia hasara na Zaidi ya yote kupata matokeo mabovu katika umwagiliaji shambani!
4. Utunzaji na marekebisho mabovu ya miundo mbinu ya umwagiliaji iliyopo.
Mashamba ya umwagiliaji yanakusanya wakulima wa chini na kuwawezesha kulima katika miundo mbinu ambayo imeshaandaliwa. Tanzania kuna schemes nyingi za umwagiliaji na kuna shemes ambazo mpaka sasa hazifanyi kazi na nyingine zinafanya kazi chini ya kiwango kutokana na uharibifu na matengezo hafifuhali inayopelekea kudorora kwa umwagiliaji na uzalishaji kwa ujumla.
5. Soko la mazao.
Dhumuni la umwagiliaji na kuzalisha kwa faida na kwa kutumia maji kwa kiwango kinachohitajika bila kupoteza maji. Ni mara nyingi unakuta mkulima ambaye aliwekeza pesa nyingi katika miundo mbinu ya umwagiliaji na kufanikiwa kuzalisha mazao ila mwisho wa siku soko linakua duni na kupelekea hasara kwa mkulima!
6. Utumiaji wa technolojia duni katika umwagiliaji.
Kutokana na ukweli kwamba wakulima wengi ni maskini, wengi wanalazimika kutumia umwagiliaji wa mifereji ambayo kwa uhalisia inapelekea upoevu mwingi wa maji na uharibifu wa ardhi! Pia kutokana na umasikini ni wakulima wachache wanamudu kutumia njia kama umwagiliaji wa matone (drip irrigation, sprinkler and centre pivort) ambazo zinahitaji mitaji mikubwa
7. Upatikanaji wa wataalamu wa umwagiliaji.
Huwezi kuwa na huduma bora za afya kama huna ma dokta, vivyo hivyo huwezi kuwa na matokeo bora ya umwagiliaji kama huna wataalamu wa kutosha wa umwagiliaji. Vijijini ambapo kilimo kinafanyika hamna wataalamu wa kutosha wa umwagiliaji nabaadhi waliopo wamejifungia ofisini au kujiingiza katika siasa hali inayopelekea ukosefu wa wataalamu wa kutosha wa umwagiliaji!
Pitia hapa kwa elimu zaidi ya umwagiliaji: Special thread: Kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)
Upepo wa pesa
G.Engineer (Irrigation and water resources)