Changamoto zetu sisi madereva wenu wa daladala

Changamoto zetu sisi madereva wenu wa daladala

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,986
Reaction score
61,204
Habari zenu,

Mimi ni mmoja wa madereva daladala hapa jijini Dar es Salaam nikiwa nafanya route ya T/Segerea kwenda Mnazi Mmoja
Kero kubwa tunayokumbana nayo ni kutoka kwa hawa ndugu zetu askari wenye njaa.

Askari hao ambao wapo karibu kila kona wamekuwa wakitupiga mabao kwa kisingizio cha kutaka kukagua gari na hivyo ili asikague inakubidi utoe (umpe rushwa) ambazo inakuwa kuanzia 5000 mpaka 10000. Nakubali kuwa tunatoa rushwa kwa sababu hela hio maarufu kama bao inaingia mfukoni mwake.

Cha kuumiza ni kuwa kwa sasa askari wamekuwa wengi na kila mahali hivyo kwa siku unajikuta umekula mabao hata manne. Jioni unamaliza hesabu ya bosi unajikuta na posho shilingi 15000 mgawane na konda wako. Hivi jamani hii ni halali kweli abiria wetu? Na hapo sijagusia 30000 kama cheti ambayo huwa tunapigwa kama faini pale tunapofanya makosa madogo.

Mfano mimi jana nimepigwa vyeti viwili jumla 60000 alafu nikachezea na mabao mawili 10000, bosi anataka umfikishie hesabu yake 100,000. Hapo bado hujaweka mafuta kwa hio tunajikuta tunakomaa sana kwenye kazi mpaka usiku bila maslahi

Ningetamani sana mamlaka husika ikataze haya mabao tunayopigwa na askari kwani hayana faida yanatuumiza sisi ni bora hio 5,000 tunayowapa tuwe tunawagaia hata watoto yatima wasiopata hata chakula.
 
Na mikwara yenu yooote kwa wanafunzi kumbe mna wababe wenu?

Kama hamwezi kujisimamia heri mwendelee kunyooshwa.

Mkuu ebu vaa viatu vya jamaa hafu ujiulize hayo maswal.kuipata lak ya tajir bado uipate 70-90 elfu za mafuta ndo ubaki na posho hapo chukulia hujapigwa bao.ndo maana wanapunguza idad ya wanafunzi
 
Mm ni mmiliki wa daladala na pia nimeshaendesha daladala sana!naujua uchungu wa madereva daladala sio mchezo!sema haina jinsi ni kuvumilia tu na kutafuta urafiki hewa ili mara nyingine wanakukaushia
 
Poleni sana Madereva tatizo lenu hamna msimamo wa pamoja, pia jaribuni kupunguza makosa yasiyo ya lazima mfano kupakia na kushusha abiria sehemu ambayo hamna kituo.
 
Poleni sana Madereva tatizo lenu hamna msimamo wa pamoja, pia jaribuni kupunguza makosa yasiyo ya lazima mfano kupakia na kushusha abiria sehemu ambayo hamna kituo.
Ni kweli mkuu lakini dah aisee too much ungejua tunavoondoka bila hata posho
 
Kutokuvaa uniform, kutoka nje ya mstari aka overtaking kushoto, kukatiza route, mashindano ya kifala na madereva wengine wa daladala, kwa kifupi mengi mnajitakia wenyewe.

Poleni sana Madereva tatizo lenu hamna msimamo wa pamoja, pia jaribuni kupunguza makosa yasiyo ya lazima mfano kupakia na kushusha abiria sehemu ambayo hamna kituo.
 
Piganeni mpate mishahara kwa mwezi hiyo hesabu ibaki tu kama target kwa siku.

Kutegemea Posho unaweza piga dash hata week nzima
kwa mfano mimi na bosi wangu tumekubaliana kila mwezi atakuwa ananipa laki 2 kama mshahara lakini hali hii haipo sawa kwani madereva wengi zaidi hata ya 70% hawana mikataba ya namna hio wengi wanaendesha kama day worker
 
Back
Top Bottom