Changamoto za kwenye mahusiano

Changamoto za kwenye mahusiano

lup

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
2,514
Reaction score
2,744
Kwa wale watu kwa ujumla wanaoingia kwenye mahusiano hasa ya kudumu, yanaweza kuwa ndoa au ya mwelekeo wa ndoa ni vyema tukawa tumejiandaa kwa lolote litakalotokea na kulichukulia hata kama ni nzito namna gani.

Kumbuka hakuna kitu kisichokuwa na mapito au changamoto kosa kubwa tunalolifanya pale tunapoingia kwenye mahusiano hayo ni pale tunapofikiri kuwa mwenzi wako huyo ni malaika na hawezi kukosea kwa namna yoyote ila wewe ndio binadamu ukikosea usamehewe na muendelee kuvumiliana ila wewe uvumilivu huna.

Pale mnapompenda mtu jua kuwa na yeye anamadhaifu yake ambayo unatakiwa kumvumilia hata kama ni ya namna gani, hata iwe ni usaliti wa ndoa ni lazima mvumilie na sio kumuacha au kumkashifu.Utakuta mtu anasema kwa jambo hili siwezi vumilia na anasahau hata yeye anavumiliwa tu.

Ni lazima tujue kuwa huwa tunakutana na watu wanaotufaa kwa yale madhaifu yetu na sio watu wakamilifu wa madhaifu yetu, yaani mfano unaweza kukuta mwanamke hawezi labda kufua nguo vizuri na wewe swala la kufua nguo sio shida sana.

So unachotakiwa kufanya sio kudharirisha na kuwa na akili mgando ya mfumo dume hapo ni kuweka mfanya kazi au fua na sio kudharirishwa kwani mke sio mfanyakazi na kuna tofauti ya mujukumu ya mfanyakazi na mke pia na heshima zao zinatofautiana, au mwanaume ni bwana mipango mzuri lakini utekelezaji wako ni ziro nawe unaweza kusimamia.Hivyo we simamia na usiwe na dharau, kwani sifa ya kwanza ya mwanamke ni utii.
 
Mkuu mbona kama unamwambia rafiki yako kupitia MMU?
rafiki hakuna mtu ninayefahamu maisha yake humu ila ni kutu nimekiwaza sana kwa juu ya mtazamo wa watu wote ambayo huwa wanaingia kwenye mahusiano na kufikilia kuwa huwa na raha tu na anapokuta mambo tofauti ndio hapo unagunduwa hakujiandaa kwa hayo.ila yeye alijiandaa kwa kufanyiwa mema tu..
 
rafiki hakuna mtu ninayefahamu maisha yake humu ila ni kutu nimekiwaza sana kwa juu ya mtazamo wa watu wote ambayo huwa wanaingia kwenye mahusiano na kufikilia kuwa huwa na raha tu na anapokuta mambo tofauti ndio hapo unagunduwa hakujiandaa kwa hayo.ila yeye alijiandaa kwa kufanyiwa mema tu..

oky poa mkuu nimekupata
 
Mtoa mada, kashaumizwa sana kwa tabia zake.

Tumhurumie Jamani.

Pole sana ndugu, ndo maisha hayo-hayako straight forward.
rafiki huwezi amini niko singo kabisa na sijaumzwa ila nafikiria kuingiamo....asante
 
haya ndio natafuta ila nikipata jamii forum itakuwa poa sana....
 
Kuna vya kuvumilia na sio vyote.
Uvumilivu una kikomo.
 
Back
Top Bottom